Jumanne, 15 Novemba 2016

Kitabu Cha Muongozo wa Shirikisho la Vyama vya waajiri katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Cha zinduliwa

                                    



                         Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali imetakiwa kushirikiana kwa karibu na jumuiya ya waajiri katika kuleta maelewano katt ya waajiri na wafanyakazi ambapo suala hilo litaleta tija na kukuza uchumi pia kuondoa migogoro,

Kauli hiyo imetolewa na Raisi wa chama cha waajiri Afrika na pia mwenyekiti wa waajiri hapa nchini Almas Maige wakati akizindua kitabu cha muongozo wa shirikisho la waajiri Afrika Mashariki jijini Arusha

Maige ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini alisema kuwa maelewano kati ya waajiri ikiwemo mipango na mazingira rafiki ya ufanyaji kazi kati yao utasaidia kuondoa matatizo na kuweka mazingira mazuri katika kuendeleza na kukuza soko la ajira hapa nchini na wanajumuiya ya Afrika mashariki.

Akitolea mfano tozo walizokuwa wakitozwa waajiri na kusema kuwa punguzo la tozo hiyo kutoka dola 1000 hadi dola 500 litasaidia katika kuboresha mazingira ya waajiri na kujiona ni sehemu ya wawekezaji hapa nchini na kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuonyesha mfano katika tozo hiyo

“Kumeokuwa na malalamiko mbali mbali ambayo serikali imeweka mikakati ya mazingira mazuri katika kuboresha maeneo m,bali mbali ya uwekezaji hapa nchini na muongozo huu niliozindua leo utasaidia nchi za Afrika mashariki kuwa na uwiano mzuri kwa waajiri na waajiriwa”alisema Maige
Nae Mkurugenzi wa Jumuiya wa waajri Zanzibar(ZANEMA) Salahi Salimu)alisema kuwa mazingira yakiboreshwa kati ya waajiri na waajiriwa na kuwa na maelewano kutaepusha migogoro ambayo ingeweza kutokea na kusababisha kutoweza kukua kiuchumi kwa wahusika na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa maelwano kati ya serikali yanaenda vizuri ila ifike mahali upanuliwe wigo mpana katika kuboresha shughuli mbali mbali za sekta hizo mbili katika kupata mafanikio ya kiuchumi katika waajiri na serikali zao.

“Uwepo wa maelewano kati ya waajiri na wafanyakazi kutajenga mazingira mazuri yatakayosaidia kukua kwa maendeleo na kuleta tija amba[po itaondoa migogoro ambayo haikuwa na lazima na hivyo kusaidia ukuaji wa kiuchumi”alisema Salahi

Mwishooooooooooooo
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni