LEMA ARUDISHWA RUMANDE MPAKA FEBRUARY 10
Kesi inayomkabili Mbunge wa
Arusha Mjini pamoja na mkewe Neema Lema leo Ijumaa February 3
imesikilizwa tena kwenye mahakama kuu ya Arusha ambapo
Pingamizi lililowekwa na wakili wa Mbunge Lema kuhusu hati ya shtaka
la upande wa jamhuri kuwa batili katika kesi inayomkabili mbunge wa
Arusha mjini Godbles Lema na mke wake Neema Lema limewasilishwa
Pingamizi limeeleza Lema na
mke wake walituma ujumbe unaosema :Tutakudhibiti kama arabuni
wanavyodhibiti mashoga"wakati hati ya mashtaka imenakiliwa ujumbe ambao
mtuhumiwa ameutumia bali ujumbe mtuhumiwa alioutuma unapaswa kupewa
jina
Wakili John Malya amesema moja
ya kosa ni kwenye hati ya mashtaka iliyotolewa na wakili wa serikali
wakati wakutaja wadhifa wa viongozi katika upande wa mbunge wameandika
mbunge badala yakuandika mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema
Malya Amesema sheria haipaswi
kubagua kwani mshtaki ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
ametajwa cheo chake na Lema ametajwa bila cheo chake
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo
John Baro amehairisha kesi hiyo hadi February 10 mwaka huu ambapo
atatolewa uamuzi pingamizi hilo.Lema amerudishwa rumande
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni