Na Ahmed Mahmoud Longido
Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa Kutenga muda wa kutoa
elimu kwa wananchama wao lengo likiwa kujua faida za vyama hivyo pamoja na
kuweka akiba na kukopa ili kuweza kuwafikia wanachama wengi zaidi hapa nchini
kukuza vipato vyao sanjari na kujiwekea akiba na hisa.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka na wa pili wa TCCIA Longido
Saccos Mwenyekiti wa Tccia wilaya ya Longido Abrahaman Konje ameitaka serikali
kutambua suala la elimu ya uwekaji akiba na uwekaji wa amana kwa watanzania suala
ambalo wengi wao bado hawana elimu hiyo.
Amesema kuwa Tatizo hilo ndio maana vyama vingi vya ushirika
vimekuwa vinaende kwa kusuasua jambo ambalo sio zuri na linaleta ukakasi kwa
wanachama katika juhudi zao za kufikia kuwa na vyama vikubwa hapa nchini
vitakavyosaidia maendeleo ya nchi na kuongeza vipato.
“Tatizo hapa nchini wanachama wengi hawana uelewa mkubwa wa
masuala ya kujiwekea akiba na Amana(HISA) hivyo kujikuta wanashindwa
kutofautisha vicoba na saccos kwa kushindwa kujiletea faida na kuendesha
familia kwa kujiwekea amana ili kuweza kuweka na kuwasaidia kusomesha watoto
wao na kujiendesha maisha”alisisitiza Konje.
Aidha Kwa Upande wake Afisa ushirika wilaya ya Longido
Japhet Mambo amewataka wataalamu wenzake kuhakikisha wanatenga muda mwingi
kuvifikia vikundi kwa ajili ya kutoa elimu ya vyama vya ushirikia kwani
amegundua vyama vingi wanachama vijijini hawana uelewa hivyo sasa ni ndio
muafaka sanjari na kuifafanua sheria namba sita ya mwaka 2013 ya vyama vya
ushirika.
Amesema kuwa wengi wa wanachama wa vyama vya ushirika
wamekuwa wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos na faida zake kwa jamii
hususani kuweka akiba na amana jambo hilo limechangia kuwepo mapungufu mengi
katika vyama vya ushirika hapa nchini.
Awali akisoma taarifa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TCCIA Longido
Saccos Ltd Flora Swai amesema kuwa chama hicho kina jumla ya wanachama 147
ambapo kina mtaji wa kiasi cha tsh.14 milion na kuwataka wanachama wenzake kuhakikisha wanajiwekea
hisa ili kuweza kufikia malengo ya chama chao.
Amesema kuwa kuanzia mwakani wataweka utaratibu wa
kuwapongeza wanachama watakaofanya vizuri na kuitaka serikali kuwafikia vyama
vya ushirika hapa nchini kuweza kutoa elimu ya uwelewa kwa wanachama wa saccos
mbali mbali ili ziwe na tija na kuongeza pato la mwananchi na taifa kwa ujumla.
“Nawasihii wanachama wenzangu kujiwekea amana na kupenda
kuuliza ili kuweza kujiletea maendeleo ambapo wengi wamekuwa pindi kunapotolewa wito wavikao
wanashindwa kufikia viwe vya serikali ama vya ushirika nawaomba muwe na moyo wa
kuitikia wito pindi unaposikia na sio kupuuzia wito”alisisistiza Swai
Mwisho…………………………………………………………..
|