Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama
Salma Kikwete akipokewa na Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa WAMA
wakati alipowasili nyumbani kwa Marehemu Mama Hulda Kibacha, Mdhamini
na Mjumbe wa Bodi ya WAMA aliyefariki dunia tarehe 28.8.2015.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye
ibada ya kumwombea Marehemu Hulda Kibacha, Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya
WAMA iliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Ada Estate tarehe
2.9.2015. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Zakhia Meghji na
kulia ni binti wa marehemu Nampombe Kibacha.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka
udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mdhamini wa Taasisi ya
WAMA Mama Hulda Kibacha aliyefariki dunia tarehe 28.8.2015 hapa Dar Es
Salaam. Marehemu Kibacha aliwahi kufanya kazi Makao Makuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini ulimolazwa mwili wa
Mama Hulda Kibacha aliyekuwa Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA.
Marehemu Hulda Kikbacha alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni tarehe
2.9.2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) kwa kushirikiana na Waziri wa
Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro (kushoto) na Mama Zakhia Meghji
(kulia) wakiweka shada la maua kwenye kaburi LA Marehemu Hulda Kibacha
aliyezikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 2.9.2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Hulda Kibacha.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, Ndugu Zakhia Meghji akitoa salamu maalum za
Taasisi hiyo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mdhamini na Mjumbe wa Bodi
hiyo Marehemu Hulda Kibacha.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Binti wa Marehemu Nampombe
Kibacha mara baada ya Mazishi ya Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA,
Mama Hulda Kibacha.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni