Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC),
 Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha 
Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya
 taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne 
Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC),
 Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu 
Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati
 wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC 
iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti
 wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na 
Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano 
baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini 
uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi
 wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa 
Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi 
mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu 
wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo 
Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti
 wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa 
Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya
 taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
 uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mkalimani
 wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa 
watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu
 wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo
 Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).
Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME 
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa 
hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi 
wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 
Oktoba, mwaka huu.
AIdha 
NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika 
kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo 
kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.
Hayo 
yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na 
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na 
wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya 
kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi 
oktoba mwaka huu.
Jaji 
Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki 
uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za 
hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi 
yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia 
hiyo.
“Vipo 
baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao  wamekuwa wakitumia muda 
mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama 
hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo” 
alisema Jaji Lubuva.
Jaji 
Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa 
vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi 
huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika 
maktaba huo.
Akifafanua
 zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya 
kuzungumza na  wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi 
tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Aidha 
Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala 
ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa 
vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya 
kiutendaji ya taasisi hiyo.
Akizungumzia
 maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi
 ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na 
masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo
 mbalimbali nchini.
Kuhusu
 Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi 
cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari 
la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki 
majina yao katika kipindi cha siku 8.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni