MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha
ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul
Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo
hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana
Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Uzinduzi
huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw.
Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa
niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz
Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa
niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
SDGs
ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami
dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila
mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika
malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa
sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
Malengo
hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs),
yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi,
ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango
wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa
mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni
balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia
lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia
ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.
Akizungumza
umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya
kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana
kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa
yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na
kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo
watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa
uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
Alisema
kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya
kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya
Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.
Pia
alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na
kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye
Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia
malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu
ya mchakato huu...”.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd
akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya
Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema
kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana
namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi
kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa
maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
Akisisitiza
umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala
Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha
malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo
ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana
na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la
umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi
kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa
wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumza
kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu
wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya
Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama
benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo
bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi
adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17
kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
Standard
Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na
inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa
atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Malengo
ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa
dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika
Januari 1,2016.
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya
uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
Mtaalam
wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia
Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
Meza
kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 (
SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers
Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan,
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez,
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo
Endelevu 17 ( SDGs).
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd
akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya
Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Kamishina
wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya
Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye
hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha
maendeleo.
Baadhi
ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs)
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye
hafla hiyo.
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana
(hayupo pichani).
Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali
na majibu.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame (
wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala
Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa
pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya
Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Sasa yamezinduliwa rasmi.
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali
wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao
vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Meza
kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi
Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha
jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Meza
kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo
Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni