MISS TANZANIA LILIAN KAMAZIMA APONGEZA UAMUZI WA BASATA


Siku chache baada ya Baraza la Sanaa la Tanzania(Basata) kulifungulia shindano la Miss Tanzania mrembo anayeshikilia taji hilo kwa sasa,Lilian Kamazima amefunguka na kupongeza uamuzi huo na kudai kwamba kufunguliwa kwake kumefungua ndoto na ajira mbalimbali hususani kwa wasichana nchini.
 
Hatahivyo,mrembo huyo amesisitiza ya kwamba Tanzania inabidi “ikaze” kujiandaa na mashindano ya dunia yanayotaraji kufanyika  mwishoni mwa mwaka huu.
 
Akihojiwa na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa jijini Dar es salaam mrembo huyo alisema kwamba bado hajapata taarifa rasmi kutoka katika kampuni inayoyasimamia mashindano hayo lakini amefurahishwa na uamuzi huo.
 
“Nimejisikia vizuri sana unajua hapo awali nikiongea na wasichana walikuwa wakiniuliza vipi kuhusu ndoto na matarajio yao”alisema Kamazima
 
Hatahivyo,alisisitiza kwamba hivi karibuni anataraji kukutana na Rais Jakaya Kikwete katika kikao maalumu na atazungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao hicho bila kufafanua nini watakwenda kujadili.
 
Naye,wakala wa mashindano ya Miss Tanzania kanda ya Kazkazini,Faustine Mwandago kupitia kampuni yake ya Mwandago Investment alitoa maoni yake na kusema kwamba anatarajin mashindano hayo yatakuwa bora hapo mbeleni endapo masharti ya Basata yakitekelezwa kikamilifu.
 
Hatahivyo,baba mzazi wa mrembo wa taji la Miss Tanzania mwaka huu,Deus Kamazima kwa upande wake alitoa maoni yake na kusema kwmaba mbali na kufurahishwa na uamuzi huo lakini alisema kwamba kufungiwa kwa shindano hilo kumeathiri ajira mbalimbali nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni