CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI ,WASEMA HADI SASA MIKATABA IMEKUWA DONDA NDUGU KWAO!

Wa pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha  waongoza Utalii Nchinni Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F. Siao
Wakizungumza na wageni mbalimbali Ambao walitembelea banda lao katika maonyesho ya Utalii yaliyo shirikisha zaidi ya makampuni  300 ya utalii,amabapo washiriki wa ndani yanchi ni 60% na yale ya nje ni 40% ambapo huwa wanafanyika lila mwishoni mwa mwezi mei .
Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.
Maongezi yakiendelea na wageni waliotembelea banda lao.Picha na Mahmoud Ahmad


Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania (TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi  ya Ngorongoro na ile ya  Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za kwenda kuangalia wanyama .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi  kwamba  changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama  kuelekea upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao upande wa pili

"Katika eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama na kuelemea  upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa na kibali cha upande mmoja tu  huwezi kuwapeleke wageni mahali wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda mrefu sasa."alisema Halifa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.

''jamani miundo mbinu ndani ya hifadhi  haswa  Tarangire na Manyara ni changamoto kubwa wakati wa mvua hakupitiki, "alisema Emanuel.

Amesema kuwa asilimia 90 ya waongoza Watalii ni waajiriwa kwenye makampuni ya Utalii ,hadi sasa mikataba yao imekuwa ni donda ndugu kwani mikataba hiyi ipo tayari lakini hakuna wakuisimamia ili ifanye kazi kama inavyohitajika.

Amesema  Waongoza watalii nchini Tanzania kilianzishwa mwaka 1999,kina jumla ya wanachama zaidi ya 3000 ,Wanachama ni 1130 ,wanachama hai waliolipa ada zao kwa mwaka 2017 ni 567 tu,amewataka waongozaji watalii hao ambao sio wanachama waamue kuiunga kwani hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto waliyonayo zaidi ya kuwa wamoja.

RC GAMBO AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WA MKOA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.     


Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.

Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.

Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji  wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.

Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.

Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.

Nae katibu tawala wa mkoa  Richard  Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.

Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.

Mkuu  wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha

TIBA MTANDAO KUANZIA OLOLOSOKWAN OKTOBA MWAKA HUU

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda wakishuhudia Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) akiweka saini kama shahidi wa makubaliano hayo.
WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine. Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Alikuwa anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha hiyo aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda kitaifa.
Katika warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradio huo mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna ya kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mradio huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO zilizoanzishwa kwa msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao.
Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016.
Wataalamu hao kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS wamekutana jana katika Kampasi ya Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana mpya kwa ajili ya utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao katika kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha Ololosokwan.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea jijini Dar Es Salaam. Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo.
Mradi huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo.
“Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira na kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua utumiaji wa teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake utakuwa mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne ya ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akitoa neno katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Warsha inayochambua dhana ya tiba mtandao ni awamu ya pili yenye kuendeleza juhudi za kutumia uwapo wa huduma hiyo Ololosokwan kwa kuwakutanisha wabunifu, wataalamu wa afya na wanateknolojia ili kudadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na baadaye kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini.
Katika warsha hiyo washiriki walipata nafasi ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Unesco na MUHAS wa ushirikiano katika utekelezaji wa dhana hiyo ya tiba mtandao. Akifafanua zaidi Dk Vumilia alisema kwamba tiba mtandao itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na wataalamu waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali zilizowasilishwa kwenye warsha hiyo.
Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen akifafanua jambo kwenye warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kulia).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya huku tukio hilo likishuhudiwa na wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS.

Picha juu na chini ni wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, pamoja na Maafisa wa Afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro wanaoshiriki warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya (kulia) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari wakati wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya.
Picha ya pamoja.

Zanzibar haibaguliwi katika EAC,


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimkaribisha Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota kutoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Kisiwani Pemba. Ushiriki na mwitikio katika semina hiyo umekuwa mkubwa kwa washiriki ambapo wameonekana kuvutiwa sana na semina hii pia wamekuwa wadadisi wazuri wa kutaka kujua zaidi fursa zinazo patikana kwenye mtangamano huo. 
Bw. Chodota akitoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Pemba. 
Sehemu ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Chodota (hayupo pichani). 
Bw. Chodota akiendelea kutoa mada yake. 
Mmoja wa washiriki Bi. Kauthari akiuliza swali mara baada ya mada kumalizika kutolewa na Bw. Chodota hayupo pichani. 
Sehemu nyingine ya washiriki wakimsikiliza kwa makini. 
Bw. Chodota akijibu swali lililokuwa limeulizwa na Bi Kauthari (hayupo pichani). 
Bw. Suleimani Haji kutoka ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar naye akitoa mada kuhusu nafasi ya Zanzibar kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza kwa makini Bw. Suleimani (hayupo pichani). 
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada na maswali yaliyo kuwa yakiulizwa na washiriki wengine. 
Mhe. Mbarouk Salim Ali Mbunge wa Jimbo la Wete akiuliza swali kwenye semina. Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Konga, Mhe. Mbarouk Ali akisikiliza kwa makini. 
Meneja wa TRA kwa upande wa Kisiwani Pemba Bw. Habibu Saleh naye akiuliza swali kwa mtoa mada, Bw. Suleimani (hayupo pichani). 
Bw. Salehe akijibu maswali hayo na kutolea ufafanuzi kwa baadhi ya mambo. 




Serikali ya Zanzibar inashiriki moja kwa moja bila ukomo katika masuala yote ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hivyo Wazanzibari wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo na kuondokana na dhana kuwa eti, Serikali yao inabaguliwa.

Akiwasilisha mada leo kuhusu ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye semina ya masuala ya mtangamano wa EAC inayofanyika Pemba, Afisa wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Bw. Suleima Haji alitoa ufafanuzi wa kina kuonesha namna Zanzibar inavyoshiriki katika EAC.

Bw. Haji alieleza kuwa licha ya Zanzibar kuwa sehemu ya muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ushiriki wake umedhihirika katika mgawanyo wa miradi ya maendeleo ya EAC, hususan miradi ya Miundombinu. Alisema Zanzibar iliwasilisha mapendekezo ya miradi 10 kwenye Sekretarieti ya EAC na kutokana na vipaumbe vilivyowekwa miradi 3 imekubaliwa na mchakato wa kuitekeleza unaendelea. Miradi hiyo ni ujenzi wa Bandari ya Marhubi kisiwani Pemba, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ununuzi wa meli kubwa zitakazosafirisha abiria na mizigo kwenye nchi wanachama wa EAC.


Aidha, kwenye miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar haijasahaulika. Zanzibar inanufaika na miradi inayofadhiliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya kukuza biashara na kupunguza umasikini katika nchi za EAC inayoitwa "East Africa Trademark" (TMEA). TMEA ambayo ni mdau mkubwa wa EAC inafadhili mradi ambao unawawezesha Wazanzibari kufanya maombi kwa njia ya mtandao ili kupata cheti cha uasili wa bidhaa. Cheti hicho ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani kinatambulisha bidhaa yako ilipotengenezwa na kupata msamaha wa kodi ya forodha inapoingia nchi nyingine za EAC. 

Mradi mwingine unaofadhiliwa na TMEA huko Zanzibar ni ule wa kuwasilisha malamiko kwa njia ya mtandao au ujumbe mfupi wa simu pale inapotokea mfanyabiashara amekumbana na vikwazo visivyo vya forodha katika kusafirisha bidhaa zake ndani ya Jumuiya. Ujumbe huo utakapopokelewa, kikwazo kilicholalamikiwa kitafanyiwa kazi na taasisi husika mara moja.

Benki ya dunia pia inaendesha mradi wa kutathmini utekelezaji wa Soko la Pamoja kwa upande wa Zanzibar. Kama inavyotambulika soko la pamoja lina vipengele vingi vikiwemo; usafirishaji huru wa bidhaa, huduma, mtaji na watu. Hivyo kuna umuhimu wa kupima namna nchi wanachama zinavyotekeleza vipengele hivyo.

Ushiriki wa Zanzibar unapatikana pia kwenye uenyeji wa taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar imebahatika kuwa mwenyeji wa Kamisheni ya  Kiswahili ya EAC. Kuwa mwenyeji wa taasisi kuna faida kubwa zikiwemo kujitangaza na ajira. Kwa upande wa ajira, Bw. Haji alisema sio tu Wazanzibari wanafaidikia na ajira za Kamisheni ya Kiswahili, bali wanapata ajira hata katika Sekretarieti ya EAC na kutolea mfano kuwa Mhasibu Mkuu wa kwanza wa Sekretarieti hiyo alikuwa Mzanzibari.

Vile vile, Zanzibar imekuwa mwenyeji wa vikao mbalimbali vya taasisi za Jumuiya. Mwaka 2010 Mahakama ya Afrika Mashariki ilifanya kikao chake Zanzibar, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) lilifanya kikao chake Zanzibar mwaka 2016 na mwezi Agosti mwaka huu utafanyika mkutano mkubwa wa masuala ya Kiswahili mjini Zanzibar. Aliendelea kusema kuwa katika Bunge la EALA la kipindi hiki, Zanzibar ina wabunge watatu, wawili wakitokea CCM na mmoja CUF. 

Alihitimisha mada yake kwa kuwasihi Wazanzibari waache fikra potofu za kujihisi kubaguliwa badala yake waunganishe nguvu kuchangamkia fursa lukuki za kibiashara zilizopo kwenye mtangamano wa EAC. Alisema Serikali ya Zanzibar inashiriki katika kila jambo ikiwemo kushiriki mikutano ya Marais. Mawaziri na Wataalamu ili kutetea maslahi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

Dar es Salaam, 18 Mei, 2017

Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini


Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kuchangamkia fursa ya fedha za kitanzania bilioni 250 zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji safi na salama vijijini (2016-2020).

Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba aliwaambia wakurugenzi wa wilaya katika semina inayofanyika mjini Morogoro jana kuwa ni halmashauri chache tu ndio zimeanza kupata fedha hizi mara baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa na wafadhili.

"Kuna fedha za kutosha katika mradi huu ukilinganisha na mwamko wa halmashauri katika kuchangamkia fursa hii ya kuongeza mtandao wa maji katika maeneo yao," alisema na kuongeza kuwa fedha hizi zinaweza kuzisaidia halmashauri kuanzisha miradi mipya na kukarabati ile ya zamani ili iweze kutoa maji kwa wakati wote wa mwaka.

Alisema moja ya sharti la upatikanaji wa fedha hizi ni ufanisi katika utekelezaji wa miradi iliyopita na ubora wa ripoti za kila mwezi kama ambavyo programu hii inavyozitaka halmashauri. Kigezo hiki ni muhimu sana katika kuvuka hatua moja hadi nyingine na kupata fungu kubwa zaidi la fedha ambalo litawezesha kutekeleza miradi mikubwa zaidi katik halmashauri husika.

Kwa mfano halmashauri zinaweza kupokea aina mbili za malipo kama vile paundi za kiingereza 50 kwa ajili ya kuendeleza kituo cha maji na fungu hili linaweza kuongezeka hadi paundi 1,500 kulingana na ufanisi wa utekelezaji katika hatua ya mwanzo.

"Ukipata paundi zaidi ya 1,500 kwa mara moja kwa miradi ya vijijini ni nyingi sana katika kuiboresha na kuifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wakati wote. Na pia fedha hizi zinaweza kutumika kuanzisha vituo vipya vya kusambazia maji hivyo kufanya mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi katika eneo husika," alisema.

Alisema ni halmashauri 57 tu ambazo ziliweza kuvuka vigezo viwili vya mwanzo kwa mwaka jana na kuweza kupata fungu kubwa zaidi la kiasi cha paundi za uingereza 5,000, fedha ambazo kwa miradi ya maji vijijini zinaweza kusaidia sana katika upatikanaji wa maji wakati wote wa mwaka.

Aliwahimiza wakurugenzi wa wilaya kuchangamkia fursa hii ya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mingi ya maji na kuifufua ile ambayo imekufa ianze kufanya kazi tena na kuongeza mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi ili kufikia adhma ya serikali ya asilimia 95 wa watu wanaopata maji katika miaka michache ijayo.

Injinia Mutazamba aliongeza kusema lengo la kuwakutanisha wakurugenzi wote nchini katika semina hiyo ni kuweza kuwaeleza kwa kina kuhusu fursa hii ya fedha za wafadhili ambazo bado zipo nyingi na zinaweza kusaidia kupunguza na hata kumaliza kabisa tatizo la maji hasa sehemu za vijijini.

Alisema programu hii ya kuongeza mtandao wa maji vijijini unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya shirika la kimataia la DFID la uingereza na serikali ya Tanzania.

Mratibu wa mradi wa usafi wa mazingira uitwao Nipo Tayari Juliana Kitira akimuonyesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Kigoma, Elinatha Elisha takwimu za hali ya usafi wa mazingira katika halmashauri yake kwenye simina inayofanyika Morogoro. Mradi huo pia unahamasisha uwepo wa vyoo bora na kunawa mikono na maji safi baada ya kutoka chooni.
Mkurugenzi wa wilaya ya Bagamoyo Fatuma Latu akiangalia msimamo wa wilaya yake katika usafi wa mazingira kupitia mradi wa Nipo Tayari chini ya Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Watoto, Walemavu na Wazee kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara Yefred Myenzi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Sabas Damian Chambasi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro. 

WAZIRI WA ZAMANI WA INDIA AMALIZA ELIMU YA SEKONDARI AKIWA GEREZANI


Waziri wa zamani wa India anayetumikia adhabu ya kifungo jela kwa rushwa amefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari akiwa na umri wa miaka 82.

Waziri huyo Prakash Chautala, aliyekuwa waziri kwa mihula minne katika jimbo la kaskazini la Haryana, alifanya mtihani wa kidato cha 12 akiwa gereza la Tihar Jijini Delhi.

Mtoto wake Abhay Chautala amesema baba yake ameamua kutumia kuutumia kwa manufaa muda anaotumikia kifungo jela kwa kusoma.


Waziri huyo wa zamani wa Haryana alitiwa hatiani kwa tuhuma za rushwa katika zoezi la kuwaajiri walimu.

WATUMISHI WA UMMA KUWENI KARIBU NA WANANCHI, BALOZI MWINYI


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi akitoa mwongozo kwa wajumbe wa semina ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea kufanyika kisiwani Pemba. Pamoja na mambo mengine amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye mtangamano.
Mbunge wa jimbo la Konga, Mhe. Mbarouk Ali akichangia jambo kwenye semina.
Sehemu ya wajumbe wakiendelea kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye semina.
Afisa kutoka Ofisi za Uhamiaji Pemba Bw. Haji Kassim Haji akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wajumbe kwenye semina juu ya upatikanaji wa Hati ya Kusafiria ya Afrika Mashariki.
Bw. Amedeusi Mzee akitoa mada kuhusu Soko la Pamoja na faida zinazopatikana kwenye soko hilo.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumz na Mbunge wa Kavuu, Dkt. Pudenciana Kikwembe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UKWELI KUHUSU MTI ULIOGOMA KUNG'OLEWA JIJINI MWANZA.


                                                                                         George Binagi-GB Pazzo @BMG
 

Wakazi wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Taharuki hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.

Zoezi la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.

Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.

Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na usambazaji wa taarifa za upotoshaji.


Zoezi la kuung'oa mti likiendelea
Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuangua licha ya kuvutwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa