JAMBAZI MREMBO AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA


Jeshi la polisi Kenya limewauwa kwa kuwapiga risasi majambazi wawili mmoja wao akiwa ni jambazi wa kike anayesemekana kuwa ni jambazi mrembo pengine kuliko wote.

Majambazi hao waliuwawa wakiwa katika eneo la Chokaa Jijini Nairobi walipopambana na polisi kwa kufyatuliana risasi, huku wenzao wawili wakifanikiwa kutoroka.

Mitandao ya jamii imemtambua jambazi huyo mwanamke kwa jina la Claire Mwaniki, ambaye alikufa mkononi akiwa ameshikilia bastola aina ya Baretta ikiwa na risasi sita.

Kamanda wa Polisi Jijini Nairobi, Japheth Koome, amesema kuwa wahalifu wengi nchini humo wanakuwa na wanawake wanaofanyanao ujambazi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni