Wananchi wa Korea Kusini wanapiga
kura kumchangua rais, katika uchaguzi ulioitishwa baada ya rais
kuondolewa madarakani kutokana na kashfa kubwa ya rushwa.
Mgombea mliberari Moon Jae-in
anaelekea wazi kuongoza kwa kura huku akichuana na Ahn Cheol-soo wa
siasa za mrengo wa kati.
Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa karibu
na dunia wakati huu wa hali tete ya uchumi na hofu ya kutokea vita na
Korea Kaskazini.
Mgombe Moon anataka kuongeza
uhusiano na Korea Kaskazini, kinyume na kiongozi aliyeondolewa Park
Geun-hye aliyekata mahusiano yote na jirani zao hao.
Wananchi wa Korea Kusini wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura kumchagua rais
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni