Na Mahmoud
Ahmad Kondoa
Watu wawili
ambao hawajatambuliwa majina yao hadi sasa wanaokiwa kuwa na umri tofauti kati
ya miaka 37 hadi 40 mmoja dereva wa Katapila lenye no za usajili T 370 BBG
lililokuwa likitengeneza barabara ya Haubi na kumgonga mtu mmoja hadi kufa na
wananchi wenye hasira kumpiga dereva huyo hadi kumuua.
Tukio hilo
limetokea wilayani Kondoa dc Kata ya Haubi kijiji cha haubi baada ya dereva
huyo ambaye jina lake halijapatikana hadi sasa kumgonga mwenda kwa miguu na
kusababisha kifo chake hapo hapo.
Mmoja wa
mashuhuda aliekuwepo eneo la tukio Mohammed Kijaji alisema kuwa tukio hilo
lilitokea majira ya saa 12;45 jioni ya tarehe 13 mwezi huu baada ya mwenda kwa
miguu huyo ambaye hakutambuliwa jina kuwa anatembea pembezoni mwa barabara na
ndipo katapila hilo kumgonga na kufa hapo hapo.
Kijaji
alisema kuwa wananchi wenye hasira kali ndipo walimvamia mwananchi huyo na
kumpiga hadi kufa dereva huyo na kusababisha mauti yake papo hapo na baada ya
kumuuwa waliendelea kuleta fujo hadi polisi walipofika eneo la tukio na
wananchi hao kutawanyika.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la
kuuwawa kwa watu wawili mmoja kwa ajali na mwingine kwa kupigwa na wananchi
hadi kufa na jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kwa mauuaji ya dereva
huyo
Kamanda
Mambosasa akizungumza kwa njia ya simu alitoa wito kwa wananchi kuacha
kujichukulia sheria mikononi na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo ambapo maiti za marehemu hao zikihifadhiwa chumba cha maiti
hospitali ya wilaya ya Kondoa.
Mwisho................................................................
|
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni