SIMANZI MAJONZI VILIO VYATAWALA JIJINI ARUSHA KATIKA ZOEZI LA KUAGA MIILI 32 YA WANAFUNZI WALIOPATA AJALI JUMAMOSI

Umati wawatu uliouthuria katika zoezi la kuaga marehemu hao
Na Woinde Shizza,Arusha

MAKAMU wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa taTanzania Samia Suluhu ameongoza maelfu ya waombolezaji katika zoezi la kuaga miili ya wanafuzi 35 wa shule ya Luck Vicent ikiwemo walimu wawili pamoja na dereva mmoja waliofariki katika ajali iliyotokea juzi eneo la Rotia wilayani karatu mkoani Arusha.
Akizungumza katika tukio hilo ambalo ni kubwa kutokea mkoani arusha na tanzania kwa ujumla alisema kuwa kama serikali walmelipokea kwa masikitiko makubwa na kwamba watajitahidi kuungana na familia zilizopoteza watoto wao ambao hata wazazi wao walikuwa na malengo mazuri juu ya kuwapatia elimu bora ,huku akiwaagiza madereva wote kuzingatia sheria za barabarani na kuepuka vilevi.
Alisema kuwa ajali nyingi zinatokana na uzembe wa madereva na hivyo kuwataka madereva wote kuwa makini pindi wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali ambazo zinqweza kuzuilika.
 

"Serikali yetu kwa sasa inapiga vita sana madereva walevi pindi wanapokuwa wanaendesha vyombo vyao hivyo naomba tu kuagiza madereva wetu kuwa makini na waadilifu kwani hata ajali kama hizi ambazo zinapoteza nguvu kazi zinatokana na vilevi vinavyotumiwa na madereva na hivyo kuleta maafa kama haya"aliongeza Samia.
Aidha aliwataka pia madereva kuhakikisha wanabeba idadi ya watu wanaolingana na uhalisia wa gari kwani wengi wao wamekuwa wakibeba idadi kubwa na hivyo kusababisha madhara mkubwa zaido pindi ajali zinazotokea mfano wa ajali hii.
Samia alitumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya elimu ,jeshi la polisi kuwa makini kuhakikisha sheria za barabarani zinazingatiwa ili kuepuka vifo vya watoto.
Awali mara baada ya kuwasili kwa miili hiyo 35 majira ya saa tano na robo uwanjani hapo Vilio ,majonzi na simanzi vilitawala katika uwanja huo huku watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa shule wakiwa wanazimia na kuwahishwa mahospitalini ili kupatiwa huduma ya kwanza.
Aidha katika zoezi hilo la kuaga miili ya wanafunzi hao serikali ya mmkoa wa arusha ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo imeweza kugaharamia shuguli zote za mazishi ya wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kutoa magari ya kusafirisha miili hiyo mpaka eneo ambalo familia imejiwekea utaratibu wa kuhifadhi miili hiyo ambapo miili 25 itasafirishwa nje ya mkoa wa arusha,huku miili 10 ikibaki kwa taratibu za mazishi ndani ya mkoa huu.
Hata hivyo akiongoza misa ya kuaga miili hiyo kwa upande wa wakristo Askofu wa kanisa la katoliki jimbo la arusha Josphat Lobulu alisema kuwa siku za mwanadamu ni chache hivyo inawapasa wanadamu kuishi maisha ambayo yanaendana na mapenzi ya Mungu.
Alisema kuwa vifo vya wanafunzi hao kimesikitisha kila mtu kwa kuwa wamekufa wakiwa malaika wa Mungu wakiwa bado wanahitajika na taifa la sasa.
Hata hivyo zoezi hilo la kuagwa kwa miili hiyo limeudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka serikalini na nje ya nchi wakiwemo waziri wa elimu wa tanzania ,waziri wa elimu kutoka nchini kenya,jaji mkuu wa mahakama ,jaji mstaafu ,waziri mstaafu lowasa na Sumaye ,viongozi wa kambi ya upinzani bungeni,madaktari kutoka nje ya nchi pamoja na wabunge mbali mbali.
 

Aidha tukio hili lilitokea mei 6 wilayani karatu ambapo wanafunzi hawa walikuwa wanenda kufanya mitihaninya ujirani mwema katika shule ya Tumaini na ndipo costa ilifeli breki na kusababisha vifo 35 na majeruhi watatu ambao ni Doreen Mshana (13),Sadia Ismaili (11) pamoja na Wilson Tarimo (11)wote wakazi wa Morombo ambapo wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount meru wakiendelea na matibabu.

Wananchi wakiwa nje ya uwanja mara baada yakushindwa kuingia ndani kutokana na wingi wa watu

Miili ya marehemu ikiwasili katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid tayari kwa zoezi la kuagwa




  Mmoja wa mwanafunzi akiwa amebebwa na wahudumu wa chama cha msalaba mwekundu mara baada ya kuzidiwa na kuanguka ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati alipokuja kuaga wanafunzi wenzake (picha zote na Woinde Shizza,Arusha)


Umati wa watu ukiwa unalia kwa uchungu
Mbunge wa viti maalumu Amina Mollel akiwa analia kwa uchungu mara baada ya kuaga miiili ya marehemu hao
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg:Jokate Mwengeloakiwa anatoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliobeba miiili ya wanafunzi hao
  Zoezi la kuaga mwili likiendelea huyu ni mmiliki blog ya fatherkidevu nae akitoa heshima za mwisho
Picha za majeneza ya wanafunzi hao 32 pamoja na walimu na dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo

  Mmoja wa Mama aliofiwa na mtoto wake akiwa analia kwa uchungu mara baada ya miili ya watoto hao kuanza kuwasili katika kiwanja cha kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni