MFUKO WA SAGCOT CTF WATOA SOMO LA KILIMO NA UFUGAJI WAKIBIASHARA KWA WAFUGAJI MKOANI NJOMBE.

 Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), John Kyaruzi (kulia), akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tano ya kilimo ufugaji wa kibiashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya mfuko huo, Dr Rosebud Kurwijila na Mkurugenzi wa Hamashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), Dk. Rosebud Kurwijila (kushoto), akifungua semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi.
 Mratibu wa Biashara wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Abdala Msambachi   akitoa elimu  kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe jana ili kufanya ufugaji wa wa kisasa utakaoinua uchumi wakati wa semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF,  Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD).
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda (kushoto),  akizungumza na wafugaji wa halmashauri yake waliohudhuria semina ya siku tano kuhusu Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya SAGCOT CTF, Dk. Rosebud Kurwijila na Katibu Mtendaji wa mfuko, John Kyaruzi.
  Baadhi ya wafugaji wakifanya wakijadiliana wakati wa  semina ya wafugaji inayolenga kuwainua kiuchumi wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe iliyoandaliwa na  Mfuko wa SAGCOT CTF.

Na Mwandishi wetu Njombe 
WAFUGAJI wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo kibiashara ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua kipato chao imeelezwa mkoani humo jana.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF kwa kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua kipato  kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara.  
Alisema hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa SAGCOT CTF  na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni mkoani Tanga 2015 mafunzo yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya kuwafanya wafugaji wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.  
“Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa kujua nini mfugaji anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji kutajirika kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo utasaidia wafugaji kufuga kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata  ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.
“Wafugaji wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini wanachokikosa ni elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF  hautatoa mkopo wa pesa pekee kwa wakulima bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema. 

Katibu Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani itasaidia wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia wakipewa mbinu ya kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa kibiashara na kwa matumizi yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja,  jamii na pia kujenga afya zao kutokana na kutumia maziwa bora. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha kwa wingi.
Nao baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika wengine waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza kuwa ufugaji wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya zao.

Mfuko wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka 2002 chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko ulitafuta wabia muhimu kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni mshirika wake katika kutoa utaalamu elekezi. (technical assistance).

NMC ARUSHA NI MALI YA SERIKALI

Image result for national milling corporation tanzania
Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI,imesema kuwa kinu cha kusaga mazao cha shirika la taifa la usagishaji,NMC ,cha Arusha hakijauzwa kama ilivyoenezwa na kitaendelea kuwa mali ya serikali na kwamba anaendesha kinu hicho ni mpangishaji na si vingine.
 
Hayo yameelezwa na msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, alipokuwa akikabidhi umiliki wa kinu hicho  cha  kusaga nafaka cha NMC ,cha Arusha kutoka kwa shirika hodhi la mali za serikali, CHC,kwenda kwa bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko. .
 
Mafuru, amesema uamuzi huo wa kukabidhi umiliki wa kinu hicho kwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni maelekezo ya serikali kwa ajili ya kukiendeleza kinu hicho na vingine vilivyopo, Mwanza, Iringa na Dodoma.
 
Amesema kuwa bodi hiyo ambayo ni mmiliki mpya itakuwa na jukumu la kukiendesha kinu hicho  itapitia mkataba wa upangaji na kampuni ya uwekezaji ya Monaban Trading Company limited kwa kuwa hiyo ni sehemu ya biashara.
 
 Amesema kabla ya kukikabidhi kinu hicho kwa mmiliki mpya  walijiridhishwa kwa kufanya  uhakiki wa vitu vilivyopo.
 .
Mafuru,amevitaja vinu vingine ambavyo havitabinafisishwa na vitabakia kuwa ni mali ya serikali ni pamoja na shirika la usagishaji la taifa NMC, Mwanza, NMC,Dodoma na NMC,Iringa ,ambavyo navyo vimekabidhiwa kwa mimiliki mpya ambayo ni bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.
 
Ameongeza kuwa kinu hicho cha NMC ,Arusha, kilipangishwa mwaka  2008 kwa kampuni ya Monaban Trading limited,kutokana na uamuzi wa serikali uliofanywa kwa wakati huo lakini sasa  mali zote za shirika la usagishaji la taifa hazitauzwa zitabakia kuwa mali ya serikali.
 
Nae Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko, John Damasi  Maige, amesema bodi hiyo itasimamia shughuli zote za kinu hicho pia watazingatia mkataba unaomwezesha mpangaji kampuni ya Monaban  kuendesha kinu hicho.
 
Amesema kuwa  mara baada ya kupitia mkataba na mpangaji ambae ni kampuni ya Monaban Trading Compan Limited,kuna mambo watakubaliana kwa masilahi ya pande zote mbili.
 
Maige, amesema kuwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko  inaendesha maghala yaliyopo Dodoma, na kufufua mashine za kusagisha zilizopo NHC Mwanza,ambacho kilikuwa ni kwa ajili ya kusagisha  na kusindika mpunga, kinu cha Dodoma kilikuwa cha kusagisha na kusindika mtama .
 
Lengo la kuvifufua  ni kuviwezesha kufanya kazi na hivyo kutoa ajira hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa .
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Monabani Trading Limited, Gerad Mandala, amesema watashirikiana na mmiliki mpya kwa kuwa kinu hicho ni mali ya serikali na kiwanda kitaendelea  kama kawaida.
 
Akawaondoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa kampuni ya Monaban ni mpangaji na ina mkataba wa muda mrefu  na itaendelea kuwa msagishaji wa nafaka na mazao mengine hivyo wananchi wataendelea kupata huduma ya unga na mahitaji mengine kama kawaida..
 
MWISHO

NHC ARUSHA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MRADI WA SAFARI CITY

Na Mahmoud Ahmad Arusha
Shirika la nyumba la Taifa limeanza ujenzi wa nyumba za mfano kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja na wananchi katika kata ya Olmort jijini hapa mradi utakaojulikana kama Safari city huku likikaribisha wananchi kuja kuwekeza kwenye mradi huo.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa shirika hilo mkoani hapa James Kisarika alisema kuwa mji huo unajengwa kwa awamu na utakuwa na vitu vyote jamii inavyohitaji ikiwemo maji, umeme na mtambo wa kuchakata maji taka.

Alisema kuwa kila kiwanja kitakuwa na huduma za bomba la maji,utengenezaji wa barabara,uandaji wa hati miliki pamoja na michoro huku katika awamu ya kwanza shirika likitoa haki za uendelezaji wa viwanja vyenye ukubwa wa mita za mraba 200-600 na yatapatikana kwa shilingi 35,000 tu kwa mita moja ya mraba.

“Mji huu ni miongoni mwa miji ya kisasa hapa nchini na utaweza kusaidia watu wa kada mbali mbali kupata kumiliki nyumba na kujenga sisi tutakuwa wasimamizi wa mradi huu”alisema kisarika

Alisema kuwa ili kuwa mmoja wa wawekezaji katika mradi huo unapaswa kufuata utaratibu kwa kuchukuwa fomu ambayo ni bure na inatolewa na shirika hilo popote hapa nchini au tembelea tovuti yao www.thesafaricity.com na utalipia asilimia 25% ya thamani ya kiwanja unachotarajia kununua.
Aidha shirika la nyumba la taifa kupitia mradi huo linatoa fursa kwa makundi mbali mbali ya wawekezaji wenye mahitaji ya uendelezaji wa nyumba za makazi kwa vipato tofauti(chini,kati,na juu) majengo ya ofisi na biashara,maduka makubwa(Shoping mall)pamoja na madogo,maeneo ya biashara,maendeleo ya viwanda vidogo vidogo,burudani na utalii,Hospital.uwanda wa elimu,sanjari na huduma zote za kijamii.
Baada ya maelezo hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi wa nyumba za mfano za mradi huo ikiwemo nyumba za makazi nafuu ambazo zitakuwa za mfano kwa nyumba za makazi ambazo wawekezaji hao watatakiwa kujenga kwa mfano huo.
Kutakuwepo na eneo la msitu pamoja na mashine maalumu ya kuchakata maji taka ambayo baada ya kuyachakata maji hayo yatatumika tena kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mradi huo.
Mwisho.

SERIKALI ,AZAKI ZASHAURIWA KUZITUMIA TAFITI KUTOKOMEZA NJAA

Image result for azaki 
 
Arusha,Serikali  pamoja na Asasi zisizo za kiraia zimeshauriwa  kuzitumia tafiti mbalimbali za masuala ya kilimo zinazofanywa na  vyuo vya elimu ya juu hapa nchini kama njia ya kusaidia kutokomeza njaa na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ushauri huo ulitolewa jana  jijini hapa na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka nchini Canada na Tanzania ambao walikuwa wakihudhuria semina ya kimataifa ya mradi wa utafiti wa kilimo utakaochukua  wiki tano kuanzia Julai 14 hadi Agosti 19 mwaka huu.

Jumla ya wanafunzi 16 kutoka Tanzania na Canada wamekutana katika semina  hiyo inayofadhiliwa na taasisi ya World Univesity Service of Canada(WUSC) kama fursa njia ya kutoa fursa kwa  wataalamu wachanga kutoka nchi hizo mbili kubadilishana uzoefu katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati mara baada ya kufunguliwa kwa semina hiyo na mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo baadhi ya wanafunzi walioshiriki semina hiyo walisema kwamba tafiti nyingi duniani zimesaidia kuleta mageuzi ya kilimo na kutatua  changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kathleen  Novelia,ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ryerson nchini Canada aliwaambia waandishi wa habari kwamba  tafiti nyingi zimesaidia mataifa mbalimbali duniani zilizotiliwa mkazo zimesaidia kutatua  kero mbalimbali hususani katika masuala ya usalama wa chakula.

“Ni jambo zuri kubadilishana uzoefu  imani yangu ni kwamba kupitia semina hii tutaibuka na njia za kukabiliana na tatizo la usalama wa chakula naamini tutakuja na mapendekezo na ushauri”alisema Novelia

Hatahivyo,Samwel Lucas ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge kilichopo  mkoani Kilimanjaro hapa nchini alisema kuwa serikali pamoja na Asasi zisizo za kiraia zinaweza kunuifaika na tafiti nyingi zinazofanya na  vyuo mbalimbali nchini kama njia ya kubuni njia rafiki katika sekta ya kilimo .

“Kuna faida nyingi kwa serikali pamoja na Azaki kwa kuwa tafiti hizi zinasaidia sana kubuni njia rafiki katika sekta ya kilimo,mbogamboga na matunda”alisisitiza Lucas

Awali mratibu wa semina hiyo kutoka taasisi ya Wusc,Christina Sudi alisema kwamba wanafunzi hao watakuwa pamoja na muda wa wiki tano kuanzia juzi kufanya utafiti katika mabadiliko ya tabia nchi,teknolojia na usalama wa chakula katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara.

Alisema kwamba utafiti huo utasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii mbalimbali hapa  nchini ambapo ripoti ya utafiti wao ikishakamilika itawasilishwa serikalini kwa lengo la kuisaidia kuleta mageuzi ya kilimo hapa nchini Tanzania na Canada.

DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA IKULU ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Said Bakar Jecha kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Septuu Mohamed Nassor kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dk.Juma Yakout Juma kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera,Ufuatiliaji na Tathmini) katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Ndg.Tahir Mohamed Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kuapishwa Viongozi mbali mbali leo Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 25/07/2016.

MAALIM SEIF KUNGURUMA TENA MAREKANI

Maalim Seif Sharif Hamad akiwasili katika uwanja wa ndege, Philladelphia. 

Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.

Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwahutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston.  

Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja.
Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uingereza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali.

Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia. 


Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.

Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar. 

Maalim Seif ambaye anafuatana na Mkuu wa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Bwana Issa Kheir Hussein, yupo nchini Marekani kuitikia mwaliko wa kuhudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democratic ulioanza jana jijini Philladelphia, mkutano ambao unatazamiwa kumpitisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa kuoitia tiketi ya Chama hicho. 

Katika mkutano wake wa hadhara na Watanzania, Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, anatazamiwa kuzungumzia zoezi zima la uchaguzi huo uliofutwa, na kusisitza madai ya Chama chake ya kurejeshewa haki yao waliyoporwa katika uchaguzi huo, na mwenendo mzima wa Demokrasia nchini Tanzania.

Itafaa kukumbusha kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kuzuru Marekani katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Mwezi uliopita, Maalim Seif alikuwepo nchini humu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kisiasa na mashirika binafsi, na kutembelea Umoja wa Mataifa ambako alifikisha madai ya Chama chake ya ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania. 

Aidha alizungumza na Watanzania waishio nchini Marekani katika jiji la Washington.

MILIPUKO MIKUBWA YATOKEA KARIBU NA UWANJA WA NDEGE WA MOGADISHU

Milipuko mikubwa iliyofuatiwa na milio ya risasi imesikika karibu na lango kuu la kuingilia uwanja wa ndege wa Jiji la Mogadishu nchini Somalia.

Moshi mzito umeonekana ukipanda juu kutoka katika eneo hilo, ambalo pia lina kambi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika.

Waandishi wa nchini Somalia wamesema milipuko hiyo imesababishwa na mabomo mawili.

MTU AWAUWA KWA KUTUMIA KISU WAGONJWA WA AKILI 19 NCHINI JAPAN

Wakazi 19 wameuwawa kwa shambulizi la kutumia kisu katika kituo cha kulelea watu wenye ulemavu wa akili katika mji wa Sagamihara nchini Japan.

Mashambulizi ya aina hiyo ni adimu mno kutokea nchini Japan, na tukio hilo limeelezwa kuwa ni baya kuwahi kutokea nchini humo tangu kupita miongo kadhaa.

Polisi wamemkamata mwanaume mmoja ambaye ni mtumishi wa zamani wa kituo hicho, ambaye alijipeleka kituo cha polisi na kukiri kufanya shambulizi hilo.
Kuna taarifa kuwa mtu huyo alinukuliwa akisema alikuwa anataka watu wenye ulemavu kutoweka kabisa.
Polisi wa Japan wakiwa katika eneo la kituo cha walemavu wa akili kilichotokea tukio hilo la kushtusha
Damu zikionekana kwenye uskani wa gari alilotumia muuaji likiwa limeegeshwa nje ya kituo cha polisi baada ya kujisalimisha mwenyewe

MICHELLE OBAMA AMPONDA DONALD TRUMP, NA KUMUUNGA MKONO BI. CLINTON

Michelle Obama mke wa rais wa Marekani amemponda mgombea urais wa Republican Donald Trump, na kumuunga mkono Hillary Clinton katika mkutano wa Taifa wa Chama cha Democratic huko Philadelphia.

Huku akishangiliwa na kupigiwa makofi na wajumbe wa mkutano huo Michelle Obama amesema lugha za chuki zinazotolewa na watu mashuhuri kwenye TV, haziwasilishi moyo wa uzalendo wa taifa hilo.

Kama hiyo haitoshi Michelle amewataka wafuasi wa chama cha Democratic kutojishusha sawa na wapinzani wao, kwani kauli mbiu ya chama hicho ni “Wao wakijishusha, sisi tunakwenda juu”.
Awali aliyekuwa mshindani mkuu wa Bi. Clinton, Seneta Bernie Sanders amewasihi wafuasi wa chama cha Democrat, kumuunga mkono Bi. Hilary Clinton.
Wanachama wa Democrat wakimshangilia Michelle Obama wakati akitoa hotuba yake
Michelle Obama akionyesha ishara ya vidole gumba baada ya kumalizi kutoa hotuba yake

WANAUME WA KIDACHI NA WANAWAKE WA LATVIA WAONGOZA KWA UREFU DUNIANI

Inapokuja suala la urefu wanaume wa Kidachi na wanawake wa Latvia imeelezwa ndio warefu kuliko wa mataifa mengine yote duniani.

Utafiti umethibitisha kuwa wastani wa mwanaume wa Kidachi ni urefu wa sentimita 183 (Futi 6), huku mwanamke wastani wa Latvia anaurefu wa sentimita 170 (Futi 5 na nchi 7).

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la eLife, ulifuatilia ukuaji wa watu katika mataifa 187 tangu mwaka 1914.

TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa, inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti nchini Brazil.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki.
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 

Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya wanariadha hao .
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliohudhuria hafla hiyo.kutoka kushoto Mkurugenzi wa Utalii na Masoko,Ibtahim Musa,Meneja Utalii Johnson Manase na Mhifadhi Vitalis Uruka.
Wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Olimpiki katika jiji la Reo De Jeneiro nchini Brazil wakiwa katika mavazi maalumu yanaotangaza vivutio vilivyoko nchini.
Mkufunzi wa Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Olyimpiki ,Francis John akizungumzia matarajio yake juu ya vijana hao.
Mmoja wa Wanariadha hao,Alphonce Felix Simbu akizungumza mara baada ya kupoke msaada kutoka  TANAPA.
Baadhi ya Wanahabari na wageni wengine waliofika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushuhudia makabidhiano hayo.
Mwanariadha Said Makuka atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Sara Ramadhan ,mwanadada pekee atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Alphonce Felix atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Fabian Joseph atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Wanariadha wanne watakao iwakilisha Tanzania katika Michuano ya Olyimpiki nchini Brazil wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Antony Mtaka ,wengine kutoka kulia ni Mkufunzi wa wanariadha hao,Francis John na anyefuatia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masokowa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.

                                        Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.
 

Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.
 

Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.
 

Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.
 

Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.
 

Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix .

KAMPUNI YA MGODI WA GEITA GOLD MINING (GGM) YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

Mkuu wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM) waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) ,Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya kundi la wapanda mlima wakiwemo wafanyakazi wa mgodi huo waliopanda kwa leongo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kiongozi wa kundi la wafanyakazi wa kampuuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining ,Kelvin Yasiwa akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuwasili wakitokea katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Balozi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akizungumza mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Lucy Mashauri(15)baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Jacob Musa (16) baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Balozi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akifurahia baada ya kukabidhiwa cheti kwa kufanikiwa kufika katika moja ya vilele vya Mlima Kilimanjaro,kilele cha Stela .
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akikabidhi vyeti kwa washiriki wengine wa changamoto hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba aliyekua mgeni rasmi katika hafla hiyo Kipi Warioba akizungumza mara baada ya kuwapokea wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining.
Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengoo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mablimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakifungua "champagne" kuonesha furaha mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimannjaro.
Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa hafla ya mapokezi yao,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba.
Watoto Yatima ambao ndio pekee walioshiriki katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika Kileleni wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba pamoja na viongozi wengine akiwemo Makamu wa Raisi wa kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining,(GGM).
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapokezi ya washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.