Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa Jumapili ijayo , yaani Julai 17, 2016
anatashiriki katika harambe ya kuchangia ukarabati na ujenzi wa maabara
na madarasa ya shule ya sekondari ya Lindi ambayo yaliungua kwa moto
wiki iliyopita. Harambee hiyo amabayo itahusisha wananchi wote wa mkoa
wa Lindi watakaokuwa tayari kuchangia, itanyika asubuhi siku hiyo.
Pichani, Waziri Mkuu akipokea
mchango wa Shilingi 2,000,000 kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Anglikan
Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almas mjini Luangwa Julai 14, 2016.
Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Wengine ni
viongozi wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya Masasi, kutoka kushoto ni
Katibu wa Sinodi ya Masasi, Janeth Lemula, Padri Kenneth Mathayo,
Joyce Liundi, Canon John Burian na Benjamin Jaali.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni