MAMLAKA
 ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za Kieletroniki za EFDs tano 
kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya 
serikali kwa kutumia mashine hizo.
 Hatua
 hiyo imetokana na agizo la  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na 
mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa.
 Akizungumza
 na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA,
 Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za 
serikali zitasaidia kutunza  kumbukumbu katika kupanga maduhuli.
“Mashine
 hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha wananchi wanaopata huduma 
wanapata risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa huduma 
wanazopata”amesema Kidata.
Aidha amesema mashine hizo ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa.
Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia.
Imeandaliwa na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akimkabadhi Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto 
Dkt. Mpoki Ulisubisya mashine tano kwaajili ya wizara yake ili kila 
wanapofanya malipo mbalimbali mapato ya TRA yakatwe.
 Kamishna
 Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akionyesha 
Mashine za Kiletroniki za EFDs ya mfano kabla ya kugawa kwa mashine tano
 katika wizara zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
jijini Dar es Salaam leo, ambazo zitakuwa kwaajili ya kukusanya mapato 
katika wizara hizo.
 Kamishna
 wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah 
Mwandumbya akitoa maelekezo ya Mashine za Kieletroniki mbele ya makatibu
 wa kuu wa wizara pamoja na wawakilishi wa wizara mablimbali jijini Dar 
es Salaam leo kabla ya Kuanza kugawa katika wizara zote za serikali.
 Baadhi ya Makatibu wa kuu wa wizara wakikabidhiwa mashine za Kieletroniki za EFDs na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
 ya wawakilishi wa wizara mbalimbali za serikali wakiwa katika mkutano 
wa kukabidhiwa mashine za Kieletroniki za EFDs jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni