Mbunge
wa Jimbo la Ilala Mh. Mussa Zungu (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano
wa hundi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yenye thamani ya
Sh. Milioni 27, sambamba na kukabidhiwa madawati 30 kwa Mwenyekiti wa
Mtaa wa karume, Haji Bechina (kulia) yenye thamani ya milioni 36, hafla
hiyo ilifanyika Mtaa wa Karume, Jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto
ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji .
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es SalaamMh. Paul Makonda akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa hafla ya kukabidhiwa mfano wa hundi kutoka kwa Mbunge wa
Jimbo la Ilala, Mussa Zungu yenye dhamani ya Sh. Milioni 27 kwa niaba ya
uchangianji wa madawati kwa kuitikia wito wa Rais Magufuli na katika
hafla hiyo mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina na yeye
alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam madawati 30 yenye dhamani ya
Sh. Milioni 36.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mh. Paul Makonda mara baada ya hafla ya kukabidhiwa hundi ya
milioni 27 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na
kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Milioni 36 kutoka kwa Mwenykiti
huyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika hafla hiyo,
kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa karume, Haji Bechina na kuanzia kushoto
ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji na Mbunge wa Jimbo la Ilala
Mh. Mussa Zungu.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina (kushoto) akimtambulisha Magreth
Mwandri (wa pili kushoto) kwa Mh. Paul Makonda ambaye alikuwa Afisa
Mtendaji wa Mtaa Karume na sasa amehamishiwa Kata ya Kitunda Mtaa wa
Kitunda Kati
Mh.
Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda akiagana na wananchi mara baada ya
kukabidhiwa mfano wa hundi yenye dhamani ya Sh. Milioni 27,na Mbunge wa
Ilala Mussa Zungu na kupokea madawati 30 yenye dhamani ya Milioni 36
toka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Karume.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa karume, Haji Bechina (kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa Paul
Makonda wakati alipofika katika hafla ya kukabidhiwa mfano wa hundi
yenye thamani ya Sh. Milioni 27 na Mbunge wa Jimbo la Ilala na kupokea
madawati 30 yenye dhamani ya Sh. Milioni 36 kutoka kwa Mwenyekiti huyo
Wananchi wakiwa katika hafla hiyo
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni