Wakazi
19 wameuwawa kwa shambulizi la kutumia kisu katika kituo cha kulelea
watu wenye ulemavu wa akili katika mji wa Sagamihara nchini Japan.
Mashambulizi
ya aina hiyo ni adimu mno kutokea nchini Japan, na tukio hilo
limeelezwa kuwa ni baya kuwahi kutokea nchini humo tangu kupita
miongo kadhaa.
Polisi
wamemkamata mwanaume mmoja ambaye ni mtumishi wa zamani wa kituo
hicho, ambaye alijipeleka kituo cha polisi na kukiri kufanya
shambulizi hilo.
Kuna
taarifa kuwa mtu huyo alinukuliwa akisema alikuwa anataka watu wenye
ulemavu kutoweka kabisa.
Polisi wa Japan wakiwa katika eneo la kituo cha walemavu wa akili kilichotokea tukio hilo la kushtusha
Damu
zikionekana kwenye uskani wa gari alilotumia muuaji likiwa limeegeshwa
nje ya kituo cha polisi baada ya kujisalimisha mwenyewe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni