Kocha
Antonio Conte ametambulishwa rasmi Stamford Bridge na kuahidi
kuifanya kazi yake kwa mapenzi na kuweza kuirejeshea makali yake
Chelsea kuweza kutinga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Conte
ameapa kuwa sasa atachapa kazi katika kuondoa mawazo ya mwenendo
mbaya wa msimu uliopita, ambao walijikuta wakiishia katika nafasi ya
kumi ya msimamo wa ligi licha ya kuwa mabingwa watetezi.
Akiongea
kwa muda wa dakika 45, katika mkutano uliopangwa kati kati ya muda wa
mazoezi, Conte amekiri kuwa itakuwa vigumu kupata mafanikio ya mara
moja katika mazingira ya ushindani mkali, ila anaimani na mbinu zake.
Kocha Antonio Conte akionyesha jezi ya Chelsea yenye jina lake
Kocha Antonio Conte akiwa amepozi katika picha iliyopingwa akiwa ndani ya uwanja wa Stamford Bridge
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni