Na Geofrey Chambua
1. Mzaliwa wa Februari 21. 1924; Komredi Robert Gabriel Mugabe Ni mtoto pekee aliyesalia katika familia yao kwani kaka zake wawili walifariki akingali mdogo sana na baba yake alitelekeza familia yao mnamo mwaka 1934 na kumlazimu mama yake kuolewa na mwanaume mwingine. Ingawa unamjua Mugabe kama Rais wa Zimbabwe ukweli ni kwamba Baba yake mzazi Gabriel Matibili ni Mmalawi aliyekua fundi seremala ila mama yake ambaye ndiye aliyemlea ni Mshona wa Zimbabwe kwa asili.
1. Mzaliwa wa Februari 21. 1924; Komredi Robert Gabriel Mugabe Ni mtoto pekee aliyesalia katika familia yao kwani kaka zake wawili walifariki akingali mdogo sana na baba yake alitelekeza familia yao mnamo mwaka 1934 na kumlazimu mama yake kuolewa na mwanaume mwingine. Ingawa unamjua Mugabe kama Rais wa Zimbabwe ukweli ni kwamba Baba yake mzazi Gabriel Matibili ni Mmalawi aliyekua fundi seremala ila mama yake ambaye ndiye aliyemlea ni Mshona wa Zimbabwe kwa asili.
2.
Kwa miaka 92 amekua akitumia zaidi vyakula vya asili ya mimea
(Vegetarian) chakula chake kikuu ikiwa ni maboga ingawa aghalabu hula
nyama pori na hasa nyama ya Simba na Tembo. Mugabe pia hatumii kileo
wala kuvuta sigara
3.
Huamka saa kumi alfajiri kila siku kwa mazoezi mepesi na hupenda sana
kusikiliza BBC baada ya hapo, huenda hii ikaelezea kwa nini husinzia
sana hata kwenye hadhara
4.
Ana jumla ya shahada SABA. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika
Chuo Kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii
zake zingine sita kwa njia ya masafa (Distance Learning) kati ya hizo
mbili za Sheria akiwa gerezani. Kazi yake ya kwanza kabla ya kujiunga
na siasa ni UALIMU na alianza kufundisha Chuo cha Ualimu Chalimbana
nchini Northen Rhodesia (Zambia kwa sasa) kisha Apowa Sekondary nchini
Ghana. Mugabe amekua akisisitiza sana katika elimu nchini mwake na
ameiwezesha Zimbabwe kuweka rekodi ya juu ya kufuta ujinga Afrika kwa
90%. Mnamo Mwaka 2005 alitunukiwa shahada ya heshima ya Uprofesa na Chuo
Kikuu cha Diplomasia huko China kwa uwezo wake wa kusomea karibu fani
zote muhimu duniani ikiwemo sheria, uchumi, historia, sayansi, sanaa,
utawala na elimu.......yasemekeana rafiki mkubwa wa maisha ya Mugabe
tangu utotoni ni 'Kitabu kwa sana'
5.
Upande wa michezo, Hupendelea sana Kriketi na Kisoka yeye ni mnazi wa
Chelsea ya Uingereza na Barcelona kwa Upande wa Spain na yasemekana ana
mizuka sanaya kisoka pia ...... 'Huwa nina midadi sana ninapotazama
kandanda, 'wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao
kwa kupiga mateke chochote kilicho mbele yangu”
6.
Mugabe pia ni mcheza kamari maarufu (kubeti) ingawa kisiri sana kwani
mwaka 2000 alistua wengi aliposhinda ZimDola 100,000 kwenye Bahati
Nasibu iliyoendeshwa na Benki ya Biashara (ZimBank)
7.
Mtoto wake wa tatu alimpata mwaka 1997 wakati huo Bob akiwa na miaka 73
alizaa na aliyekua karani muhtasi wake aitwaye Grace Marufu (miaka 38)
ambaye kwa wakati huo alikua mke wa mtu (mchepuko) na akalazimika
kumtaifisha kama mkewe wa TATU katika maisha yake ya ndoa
8.
Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-Bob haamini sana katika
ufuasi wa dini. Alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC,
miaka michache iliyopita, Jongwe huyu wa Afrika alikiri kwamba hata
maswahiba wake wengi humchukulia Mugabe kama mpagani tu kutokana na
mtindo wa maisha yake (life style).
9.
Tayari ameshaweka wazi nia yake ya kuwania kiti cha Uraisi mnamo mwaka
2018 ambapo panapo majaliwa atakua na miaka 94 hivyo atakua ametimiza
miaka 30 ya uraisi iliyotanguliwa na miaka 7 ya Uwaziri Mkuu (The oldest
and longest serving President in the whole world)
Aliwahi kuulizwa na waandishi wa habari
Mwandishi: Mr President, When will you say goodbye to the people of Zimbabwe? (Lini utawaambia kwa heri wananchi wa Zimbabwe?)
Mugabe: Where are they going? (Kwani wanaenda wapi?)
10.
Mugabe ambaye hujulikana sana kwa majibu na misemo yenye utata sana
hasa kwa waandishi wa habari, amewahi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha
wateule wachache wa kuwania tuzo ya amani ya Nobel ingawa hakushinda
kufuatia mfululizo wa mauaji nchini kwake kipindi hicho baada ya
kumtimua Joshua Nkomo kutoka Baraza lake la Mawaziri hali
iliyowachukiza Wandebele na kuzua mapigano ya kimbari dhidi ya Washona.
11.
Mugabe amejipatia umaarufu Barani Afrika na Kwingineko Duniani kwa
misimamo yake thabiti kiasi cha kuitwa dikteta wa aina yake (In 2007,
Parade magazine ranked Mugabe the 7th worst dictator in the world) na
hasa kupinga ukoloni mamboleo nchini mwake na pia tabia za kushiriki
mapenzi ya jinsi moja ambapo mnamo mwaka 1997 Mahakama ya nchi hiyo
ilimtia hatiani kwa makosa 11 mtangulizi wake Cannan Banana kwa
kushiriki ngono kinyume cha maumbile (sodomy). Banana ndiye Rais wa
Kwanza wa Zimbabwe.
12.
Mnamo mwaka 1975, Mugabe alichaguliwa kuwa Rais wa ZANU-PF huku
akingali anatumikia kifungo kwa chagizo kubwa la Askofu Abel Muzorewa
Mugabe
ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimia umri wa
miaka 92 mwaka huu na tayari Chuo kimoja cha utafiti nchini Uingereza
kimetaarifu Mugabe kuishi milele kutokana na mwili wake kuwa na vinasaba
ambavyo havina urafiki na mauti licha ya kuzushiwa kifo mara kadhaa.
Mnamo Februari 16 mwaka huu alinukuliwa akisema kwamba hana mpango wa kustaafu URAIS hadi 'Mwenyezi Mungu atakapomuita'
Mwandishi: Mweshimiwa Rais, huoni kwa umri wako wa miaka 89 ni wakati mwafaka wa kupumzika na kuachana na kazi?
Mugabe: Umewahi kujaribu kumwuliza swali hili Malkia Elizabeth au swali lako ni kwa ajili ya viongozi wa Kiafrika tu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni