MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAKUMBUKA WENYE UHITAJI.

Siku chache kabla ya kusherehekea Siku Kuu ya Idd, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (pichani), amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula kwa watoto ajili ya yatima pamoja na wazee mkoani Mwanza.  Na BMG
 

Jana Mhe. Mongella alikabidhi mbuzi 20, mafuta ya kula ndoo 20, kila moja lita 20, mchele mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 50 pampja na sukari mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 25.

Vituo saba vya watoto yatima mkoani Mwanza vilinufaika na msaada huo ni Nabawi Mbugani, Markaz Riyabwa-Nyakurunduma, Markaz Sharif Said-Nyegezi, Markaz Sainaa, Islamic Yatima, Jawhary Butimba, Muuminu Kabuhoro pamoj na Masjid Noor-Nyakato huku kituo cha Wazee Bukumbi nacho kikinufaika na msaada huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa tatu kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula kwa wahitaji mkoani Mwanza, ili kusherehekea katika sikukuu ya Idd inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu.
Baadhi ya ichimburi a.k.a mbuzi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwa ajili ya kitoweo kwa watu wenye uhitaji wakiwemo yatima na wazee mkoani Mwanza ili waweze kusherehekea vyema siku kuu ya Idd.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni