Waziri
 Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu Mzee John Samwel Malecela 
amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana kufufua zao la 
Zabibu Mkoani humo kwa kuzishughulikia changamoto zinazodidimiza kilimo 
cha zao hilo.
Mzee
 Malecela pia amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kutekeleza agizo la 
Mheshimiwa Rais Magufuli la kuondoa Tatizo la njaa Mkoani Dodoma kwa 
 kuzifuatilia skimu zote za kilimo zinazolegalega na zile zilizokosa 
uongozi imara.
Aliyasema
 hayo mwishoni mwa wiki walipoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. 
Jordan Rugimbana kwenye ziara ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya zabibu 
ya Chinangali II yenye jumla ya ekari 1,250 iliyopo Chamwino ambayo kwa 
sasa inalegalega na kumtaka Mkuu wa Mkoa kuingilia kati kunusuru skimu 
hiyo inayokabiliwa na changamoto za kukosa uongozi imara na uendeshaji 
wa kilimo usio zingatia kanuni za kilimo bora.
Aliitaka
 serikali kusaidia wakulima wa chama cha CHABUMA wanaomiliki skimu hiyo 
ya zabibu ya Chinangali ili waweze kuanzisha kiwanda cha kusindika 
mchuzi wa zabibu na kusema kuwa kufanya hivyo kutawaepusha wakulima wa 
zabibu dhidi ya wafanyabiashara walanguzi wanaowalalia wakulima wakati 
wa mavuno ya zabibu.
Katika
 hatua nyingine, Mzee Malecela amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kuondoa 
tatizo la njaa kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kufufua skimu zote zilizokufa 
na zile zinazolegalega Mkoani hapa ili ziweze kuzalisha chakula na 
ametaka mkazo mkubwa uwekwe kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Mkoa 
wa Dodoma una maji mengi chini ya ardhi.
Amesema
 serikali inaingia gharama kubwa sana kuanzisha skimu za umwagiliaji 
lakini nyingi zinakosa ufuatiliaji na uongozi imara matokeo yake 
zinakufa akitolea mfano skimu ya Mgangalenga iliyopo Mpwayungu Chamwino 
yenye zaidi ya Ekari 20,000. Kwa mujibu wa Katibu Tawala msaidizi wa 
Uchumi na Uzalishaji Bi. Aziza Mumba amesema Mkoa wa Dodoma una skimu za
 umwagiliaji zipatazo mia tatu (300).
Mkuu
 wa Mkoa Mheshimiwa Rugimbana amekubali ushauri huo na kuahidi kuufanyia
 kazi kwakuwa agizo la kuondoa njaa ni moja ya maagizo aliyopewa na 
Mheshimiwa Rais Magufuli. Amesema kwanza atakua mlezi wa skimu ya zabibu
 ya Chinangali, na kuwa atafanya jitihada za kutafuta wafadhili kwa 
lengo la kuwezesha mradi wa kiwanda cha kusindika mchuzi wa zabibu.
Pamoja
 na   kutembelea skimu hiyo ya Chinangali, Mkuu wa Mkoa ameahidi 
atazitembelea skimu zote mia tatu (300) ili kubaini changamoto za kila 
skimu na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi ili zote ziweze kuzalisha kisasa 
na kusaidia katika jitihada za kuondoa tatizo la njaa.
Rugimbana
 amesema tayari ameshaunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia 
masuala ya uzalishaji katika miradi ya Kilimo na Mifugo na moja kati ya 
jukumu kubwa alilokipa kikosi kazi hiko ni kubaini changamoto za skimu 
hizi za umwagiliaji, kuhakikisha kinakua nazo karibu na kuzijengea uwezo
 ikiwa ni pamoja na kuimarisha uongozi wa skimu hizo zote na uzalishaji 
kwa ujumla.
Waziri
 Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela 
akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana 
wakisalimiana na Viongozi wa skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo 
Chinangali II Chamwino wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa 
wiki.
Afisa
 Kilimo Wilaya ya Chamwino Ndg. Godfrey Mnyamale akiwasilisha taarifa ya
 mradi wa skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II kwa mkuu wa 
Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mzee Malecela (hawapo pichani) wakati
 walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa 
skimu hiyo.
Waziri
 Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela 
akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana (kushoto) changamoto 
zinazo didimiza kilimo cha Zabibu Dodoma na kumtaka kufanya kila awezalo
 kufufua zao hilo sambamba na kuondoa tatizo la njaa Dodoma wakati 
viongozi hao walipotembelea skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali
 II mwishoni mwa wiki.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiahidi kufufua zao la zabibu 
Mkoani humo na kuondoa tatizo la njaa kwa kufufua skimu zote za 
umwagiliaji zinazolegalega na kukosa uongozi imara wakati akizungumza na
 viongozi wa skimu ya umwagiliaji wa Zao la zabibu iliyopo Chinangali II
 Chamwino mwishoni mwa wiki.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa
 Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua mitambo ya kusukuma 
maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II 
Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa 
wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa
 Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua miundombinu ya maji 
kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino 
wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine
 ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri
 Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela na 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana wakikagua shamba la zabibu la 
Chinangali II Chamwino linalotumia teknolojia ya Umwagiliaji wa matone 
wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine
 ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri
 Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela 
akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana jinsi tatizo la 
fangasi linavyoshambulia zao la zabibu wakati wakikagua shamba la zabibu
 la Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo
 mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Sehemu
 ya Skimu ya zabibu ya Chinangali II iliyopo Chamwino inayotumia 
teknolojia ya umwagiliaji wa matone, kwa sasa skimu hiyo na nyingine 
baadhi Mkoani humu zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto 
kadhaa wa kadhaa ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana 
ameahidi kuzitafutia ufumbuzi.
Sehemu
 ya kitalu cha kuzalisha miche kwenye Skimu ya zabibu ya Chinangali II 
iliyopo Chamwino, kwa sasa skimu hiyo na nyingine baadhi Mkoani humu 
zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto kadhaa wa kadhaa 
ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kuzitafutia
 ufumbuzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni