RAIS OBAMA ATAKA WATU WEUSI NA POLISI KUACHA UHASAMA

Rais wa Marekani Barack Obama amewasihi polisi na jamii ya watu weusi kuboresha mahusiano yao, na kusema haipaswi kuwepo kwa misimamo ya "Sisi dhidi yao".

Rais Obama ametoa kauli hiyo katika kongamano lililoandaliwa na kituo cha habari cha ABC, kujadili ubaguzi na sera, kufuatia kuongezeka hofu za kibaguzi hivi karibuni.

Wiki iliyopita mtu mwenye bunduki aliwapiga risasi na kuwauwa polisi watano huko Dallas katika maandamano ya "Maisha ya Weusi Yana Thamani".

Mtu huyo Micah Xavier Johnson aliwaambia polisi alifanya kitendo hicho baada ya kukerwa na tukio la polisi kumuua kwa kumpiga risasi mwanaume mmoja mweusi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni