WAZIRI MKUU MPYA WA UINGEREZA TERESA MAY APANGA BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI

Michael Gove ametimuliwa katika wadhifa wa waziri wa sheria na nafasi yake kuchukuliwa na Liz Truss wakati Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Bi. Theresa May akiunda serikali yake mpya.

Waziri wa Elimu Nick Morgan naye ameachwa nje ya baraza hilo, na nafasi yake ikichukuliwa na aliyewahi kuwa waziri wa maendeleo ya kimataifa Justine Greening.

Waziri wa Utamaduni John Whittingdale naye pia ametoswa, huku waziri wa afya Jeremy Hunt akibakia kwenye wadhifa wake huo.

Hapo jana Boris Johnson aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje katika hatua ya kushangaza iliyochukuliwa na Waziri Mkuu Bi. May.
                                       Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni