Arusha,Serikali pamoja na Asasi zisizo za kiraia zimeshauriwa kuzitumia tafiti mbalimbali za masuala ya
kilimo zinazofanywa na vyuo vya elimu ya
juu hapa nchini kama njia ya kusaidia kutokomeza njaa na kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi.
Ushauri huo ulitolewa
jana jijini hapa na baadhi ya wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu kutoka nchini Canada na Tanzania ambao walikuwa
wakihudhuria semina ya kimataifa ya mradi wa utafiti wa kilimo utakaochukua wiki tano kuanzia Julai 14 hadi Agosti 19
mwaka huu.
Jumla ya wanafunzi 16
kutoka Tanzania na Canada wamekutana katika semina hiyo inayofadhiliwa na taasisi ya World
Univesity Service of Canada(WUSC) kama fursa njia ya kutoa fursa kwa wataalamu wachanga kutoka nchi hizo mbili kubadilishana
uzoefu katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
Wakizungumza kwa
nyakati mara baada ya kufunguliwa kwa semina hiyo na mkuu wa wilaya ya
Arusha,Mrisho Gambo baadhi ya wanafunzi walioshiriki semina hiyo walisema
kwamba tafiti nyingi duniani zimesaidia kuleta mageuzi ya kilimo na
kutatua changamoto ya mabadiliko ya
tabia nchi.
Kathleen Novelia,ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu
cha Ryerson nchini Canada aliwaambia waandishi wa habari kwamba tafiti nyingi zimesaidia mataifa mbalimbali
duniani zilizotiliwa mkazo zimesaidia kutatua
kero mbalimbali hususani katika masuala ya usalama wa chakula.
“Ni jambo zuri
kubadilishana uzoefu imani yangu ni
kwamba kupitia semina hii tutaibuka na njia za kukabiliana na tatizo la usalama
wa chakula naamini tutakuja na mapendekezo na ushauri”alisema Novelia
Hatahivyo,Samwel Lucas
ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge kilichopo mkoani Kilimanjaro hapa nchini alisema kuwa
serikali pamoja na Asasi zisizo za kiraia zinaweza kunuifaika na tafiti nyingi
zinazofanya na vyuo mbalimbali nchini
kama njia ya kubuni njia rafiki katika sekta ya kilimo .
“Kuna faida nyingi kwa
serikali pamoja na Azaki kwa kuwa tafiti hizi zinasaidia sana kubuni njia
rafiki katika sekta ya kilimo,mbogamboga na matunda”alisisitiza Lucas
Awali mratibu wa semina
hiyo kutoka taasisi ya Wusc,Christina Sudi alisema kwamba wanafunzi hao
watakuwa pamoja na muda wa wiki tano kuanzia juzi kufanya utafiti katika
mabadiliko ya tabia nchi,teknolojia na usalama wa chakula katika mikoa ya
Arusha,Kilimanjaro na Manyara.
Alisema kwamba utafiti
huo utasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii mbalimbali hapa nchini ambapo ripoti ya utafiti wao ikishakamilika
itawasilishwa serikalini kwa lengo la kuisaidia kuleta mageuzi ya kilimo hapa
nchini Tanzania na Canada.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni