MTOTO AGUNDULIKA AKIWA AMEFUNGIWA NDANI NA WAZAZI WAKE KWA MIAKA 11 MBEYA


Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Kata ya Ilemi jijini Mbeya mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili akiwa amelala ndani ,kwa zaidi ya miaka 11 sasa kwa kile kinacho elezwa kuwa ni kufichwa ndani na wazazi wake ili kuondoa aibu ya familia.

Mahali anapo lala kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha aibu ya familia.

Kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa amebebwa na shangazi yake Stella Mbuligwe mara baada ya kutoka kufanyiwa usafi wa mwili kutokana na wazazi wake kutoweza kutoa ushirikiano kwa kijana huyo.

Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Ilemi jijini Mbeya ambaye anatatizo la akili na ulemavu wa viungo akipelekwa ndani na shangazi yake ,Stella Mbuligwe mara baada yaa kufanyiwa usafi na kupatiwa chakula.

Na Emanuel Madafa, Mbeya

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili, amegundulika kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.

Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amejulikana kwa jina la Fredrick Emmanuel ametajwa kuwa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni