Wanaumoja wakiwa katika picha ya pamoja katika lango kuu la kuingia chuoni hapo kwa kampasi ya mjini kabla ya kuelekea kituoni
Wana UKI wakikaribishwa na kupewa maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bw.Lazaro Edward mara tu walipowasili
Mwenyekiti
wa vijana CCM mkoa wa Kilimanjaro Juma Raibu (Kushoto) akiwa na Rais wa
Serikali ya wanafunzi SMMUCo Edgar Nziku ambao wote ni wana
UKI wakiwa na watoto kituoni hapo.
Umoja wa Kijamii (UKI) ulioanzishwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha
Stefano Moshi Memorial University wenye lengo la kuitumikia jamii kwa
kujitolea kupunguza changamoto za ukali wa maisha katika jamii ulipata
fursa ya kukitembelea kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji
maalum cha Kilimanjaro Orphanage Centre kilichopo kata ya Pasua wilaya
ya Moshi mjini mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumzia
historia yao, Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Lazaro Edward alisema kituo
hicho kinachopokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea
kwasasa kinalea watoto wapatao 79 huku watano kati yao wakiwa ni
waathirika wa virusi vya Ukimwi kueleza kuwa changamoto kubwa
inayowakabili ni idadi ya vitanda pamoja udogo wa eneo lakini
wanatarajia kukihamisha kituo hicho baada ya ujenzi wa kituo rasmi
kukamilika.
Wanaumoja
wa UKI wanaosoma kozi mbali mbali walikuwa na wasaha mzuri wa kucheza ,
kuongea pamoja na kuwakabidhi zawadi watoto hao zenye thamani ya
shilingi laki tatu.
Akieleza
lengo la kukitembelea kituo hicho mwenyeketi wa umoja huo
Bw. Msiyaki Kuruchumila mwanafunzi wa Elimu na
Usimamizi wa Bishara alisema kuwa hii ni sehemu ya muendelezo wa
majukumu yao kama Umoja wa Kijamii na hivyo bado safari yao
kuelekea kujitoa kwa jamii bado ni ndefu.
Mwandishi
wetu alipotaka kujua kwanini kuhusu umoja huu kuwa umejikita zaidi
katika chuo cha SMMUCo na je yapo malengo zaidi ya kuutanua,Bw.
Kuruchumila alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuuneza katika vyuo
vyote katika mkoa wa Kilimajaro na wanajitahidi hili liwe limekamilika
kabla ya mwezi wa kumi na moja mwaka huu.
"Sisi
kama SMMUCo peke yetu hatuwezi kwa kuwa jamii inamahitaji mengi na
baada ya kuridhika kuhusu uimara wetu ndani ya SMMUCo tumeanza mchakato
kuhakikisha UKI inasambaa katika vyuo vyote hapa Moshi ikiwa ni MOCu,
KCMC,MWECAU na MWEKA" alihitimisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni