SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, LAWATAKA VIJANA KUZIDISHA UADILIFU NA UZALENGO KUKIDHI LENGO LA RAIS DK. MAGUFULI



Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Daniel Zenda akizungumza wakati wa kufungwa Kambi ya Vijana 219,  waliokuwa katika kambi ya kukuza Uzalendo, iliyowekwa Hombolo mkoani Dodoma.

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu nchini, limewahimiza Vijana kuzidisha uadilifu na uzalendo ili kufikia malengo yatakayoakisi CCM mpya na Tanzania mpya, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli.

"Ili matakwa haya ya Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama, yaweze kufikika, ni lazima  Watanzania  hasa sisi vijana, tubadilike, kifikra na kimtazamo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea", alisema Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo, Daniel Zenda, wakati wa kufungwa kambi maalum ya siku tatu ya Vijana kutoka  vyuo mbalimbali, nchini, jana, Hombolo, mkoani Dodoma.

Zenda alisema, mabadiliko ya kifikra, mtazamo na kiutendaji, ndivyo vitakavyoonyesha udhati wa vijana na Watanzania kwa jumla katika kuendelea kumuunga mkono, Rais Dk. Magufuli, katika jitihada zake za kuiletea Tanzania mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji kwa kushika misingi ya kuinua uchumi huku akipambana na uzembe na ubadhirifu.

Zenda, aliwapongeza vijana 219, walioshiriki katika kambi hiyo, akisema, mafunzo ya ukakamavu na yale ya kujenga utaifa, waiyopata kwa muda wa siku tatu hadi kufikia jana, yatawasaidia sana, katika kutambua nafasi yao katika kulitumikia taifa kwa uadilifu na uzalendo mkubwa.

Aliwataka Wanashirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu katika mikoa mbalimbali kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni kutekeleza maagizo  yanayotaka kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha anashiriki shughuli kama hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.

Zenda aliipongeza Viongozi wa Shirikisho katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma ambao tayari wamekuwa wakishirikiachama na wanachama na wananchi kwa jumla katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi na kujitolea damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 5, 2017.

Kambi hiyo ya Hombolo ilifungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainabu Abdalla Issa, ambaye akifunga kambi hiyo alisema, kwa kuwa CCM imekuwa ikionyesha kuwajali vijana kwa kuweka mipango mbalimbali ya kuwaendeleza sambamba na watanzania wengine, basi hawana budi nao kuhakikisha CCM inazidi kuimarika na kuwa CCM mpya.
HABARI KATIKA PICHA

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Zainabu Abdallah Issa, akizungumza wakati wa kufunga Kambi ya Vijana 219 wa Shirikisho hilo, jana, Hombolo mkoani Dodoma.
 Vijana walioshiriki Kambi wakiwa ukumbini
 Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula alipotembelea kambi ya Vijana 219 wa Shirikisho hilo, Hombolo mkoani Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo Daniel Zenda
 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula akishiriki kuimba wimbo wa Uzalendo, alipowasili katika ukumbi kwenye kambi ya Vijana wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, iliyokuwa imewekwa Hombolo mkoani Dodoma. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo Daniel Zenda
 Vijana waliokuwa katika kambi ya Uzalendo Hombolo mkoani Dodoma wakiwa ukumbini wakati wa kufunga kambi hiyo jana.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Philip Mangula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, alipotembelea kambi hiyo
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Zainab Abdallah Issa akijadili jambo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo Daniel Zenda wakati wa kufungwa Kambi ya Vujana wa Shirikisho hilo Hombolo mkoani Dodoma jana
 PICHA ZOTE KWA HISANI YA SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU.

MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya Upandaji MitiKimkoa  .


Na Emanuel Madafa,Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14  kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.

Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60  kwa kufuata sheria ya mita 60.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji  miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.

Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa  mazingira katika maeneo yot.


"Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala.


Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji  kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku.


 "Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka  katika kila halmashauri mkoani humo  ambapo mwezi juni mwaka huu  kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema .


Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Mwisho

Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017

Afisa habari na Mawasiliano Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)akichukua matukio katika tukio hilo la kilele cha upandaji miti kimkoa katika safu ya Mlima Mbeya Itagano.

Mkutano ukiendelea.........

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti katika kilele cha Upandaji kimkoa katika chanzo cha Maji Hanzya Kata ya Itagano.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kushoto akiteta jambo na Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika Safu ya Mlima Mbeya eneo la Chanzo cha maji cha Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya

Askari wa JKT Itende Mbeya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA) na baadhi ya watumishi halmashauri ya jiji la Mbeya wakiendelea na zoezi la upandaji miti katika Safu ya Mlima Mbeya katika Chanzo cha Maji Hanzya Itagano Jijini Mbeya .Picha Fahari News na JamiiMojablog.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF PROFESA LIPUMBA KWA NYAKATI TOFAUTI JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto), ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipomtembelea ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

                                                 ...............................................................


Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuwa inampango wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Malika Berak ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Balozi huyo amesema mkopo huo itaiweza na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na miradi ya umeme. 

Kuhusu uandaaji wa kongamano la uwekezaji nchini, Balozi Malika Berak amemweleza Makamu wa Rais kuwa maandalizi ya kongamano hilo kubwa la Kibiashara linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa yanakwenda vizuri. 

Balozi huyo amesema kuwa kongamano hilo ambalo litakuwa la Kikanda litajadili kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.

Balozi Malika Berak amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa kongamano hilo la kibiashara litawakutanisha pamoja wafanyabiashara  Watanzania na wenzao wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.




Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake hapa nchi kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya umaskini nchini.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini Malika Berat kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na Ufaransa.

Makamu wa Rais pia amepongeza jitihada za Serikali kupitia Ubalozi wake hapa nchini za kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano la kibiashara hapa nchini ambalo litatoa fursa kubwa kwa watalaamu wa sekta mbalimbali nchini kukutana na kujadiliana mambo kadhaa ikiwemo fursa za uwekezaji nchini.

 Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt John Magufuli inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kupambana na vitendo vya rushwa kama hatua ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.
Makamu wa Rais amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka kusaidia mchakato huo kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda nchini.

MHE WAZIRI MKUU AKIFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA RCC MKOA WA DODOMA


Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma ( Picha na PMO)

BALOZI SEIF AKAGUA BANDARI YA MKOANI ZANZIBAR


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Katikati akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma kushoto yake akikagua Bandari ya Mkoani inayokusudiwa kutoa huduma za Kimataifa.

Balozi Seif kati kati akiwa pamoja na Mkuu waMkoa Kusini Pemba wakiangalia mandhari ya Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba akimalizia ziara yake ya siku Tatu Kisiwani Pemba.

Balozi Seif akitembezwa katika eneo linalotarajiwakujengwa kwa ajili ya uwekwaji wa makontena pembezoni mwa Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifa akiambatana na Uongozi wa Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani kukagua shughuli za huduma za Afya zinazotolewa katika Hospiytali hiyo. 
Balozi Seif akiagiza uwajibikaji uliobora kwawafanyakazi wa Hospiali ya Abdulla Mzee alipokagua Kitengo cha X RAY.

Balozi Seif akionyesha kufarajika kwake na huduma zauchunguzi wa Maabara zinazotolewa na Hospitali ya Abdulla Mzee wakati alipokagua kitengo cha Maabara Hospitalini hapo.


Daktari Mkuu wa Hospitali ya Abdulla Mzee MkoaniDr. Haji Mwita Haji akielezea changamoto wanazopambana nazo watendaji wa Hospitali hiyo wakati wanapotoa huduma za Afya kwa Wananchi.Picha na – OMPR – ZNZ.

Shirika la Bandari Zanzibar limejipanga kuimarisha miundombinu yake
katika kuona Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba inatoa huduma zinazokidhi kiwango cha Kimataifa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania { TRA } tayari imeshatoa idhini na kutangaza kwamba Bandari ya Mkoani Pemba inaweza kutoa huduma za Kimataifa ikiwemo shughuli za kupokea na kusafirisha Makontena kutokana na kukuwa kwa biashara katika Kisiwa hicho.

Msaidizi Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Tawi la Pemba Nd. Hamad Salum alieleza hayo wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi  Seif alipofanya ziara ya kukagua shughuli za Bandari hiyo akimalizia ziara yake ya siku Tatu Kisiwani Pemba.

Ndugu Hamad alisema Uongozi wa Shirika la Bandari tayari umeshaanza
hatua ya kufanya maboresho ya Baboya, Umeme pamoja na huduma za Maji
safi na salama yaliyokwenda sambamba na Ununuzi wa Krini ya Kuteremshia Vitu vizito Bandarini.

Alisema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa Utafiti wa Kitaalamu wa kuiangalia upya Banadari hiyo uliofanywa mwaka 2016 kwa lengo la kuunga mkono maamuzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania. Msaidizi Mkurugenzi huyo wa Shirika la Bandari Tawi la Pemba alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Bandari ya Mkoani hivi sasa inaendelea kupokea Meli za mizigo na Abiria kutoka Unguja na Mombasa Nchini Kenya.

Alisema kwa sasa Bandari hiyo imeshapokea meli zenye uwezo wa kubeba
Tani 200 kutoka Unguja na Makontena 300 yenye ujazo wa Tani 300 kutoka
Pemba licha ya kwamba bado wapo baadhi ya Wafanyabiashara wenye
kigugumizi cha kuteremsha makontena yao moja kwa moja kutoka nje ya
Zanzibar.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma
alisema kwa Vile Shirika lake tayari limeshanunua Krini Moja ya kuteremshia Mizigo, uwezo wa kushusha makontena ya wafanyabiashara katika Bandari ya Mkoani upo na kinachohitajika kwa sasa ni kuona Mizigo ya Wafanyabiashara kutoka Nje ya Zanzibar inakwenda Pemba moja kwa moja badala ya kupitia kisiwani Unguja na Mombasa Nchini Kenya.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema wazo la Uongozi wa Shirika hilo la Bandari kuimarisha Bandari ya Mkoani ni jema na la msingi kwa sababu litasaidia kufungua njia zaidi za Kibiashara kati ya Visiwa vya Zanzibar na Mataifa mengine Duniani.

Balozi Seif alisema shughuli za Bandari ni miongoni mwa maeneo ambayo
Serikali Kuu inategemea kuongeza Mapato yake sambamba na kupanuka kwa
fursa za ajira zitakazowanufaisha Wananchi Wazalendo hasa Vijana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Shirika la Bandari na washirika wake vikiwemo vyombo vya Ulinzi kuhakikisha kwamba udhibiti wa uingiaji na utokaji katika maeneo ya Bandari unaimarishwa ipasavyo.

Alisema wapo baadhi ya watu hutumia harakati za wasafiri kuingiza mambo yao ikiwemo usafirishaji wa bidhaa haramu lakini pia uingiaji wa wageni wasiozingatia sheria na utaratibu uliowekwa na Taifa wa Uhamiaji.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba kuangalia huduma za Afya zinazotolewa na watendaji wa Hospitali hiyo.

Daktari Mkuu wa Hospitali ya Abdulla Mzee Dr. Haji Mwita Haji alimueleza Balozi Seif kwamba mazingira bora ya miundombinu ya Vifaa, Majengo na watendaji yamepelekea Wananchi wa Kisiwa cha Pemba kuwa kimbilio la kutaka kupata huduma za Afya.

Hata hivyo Dr. Haji Mwita alisema zipo changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo pamoja na Watendaji wake akazitaja baadhi kuwa ni pamoja na umbali wa Makaazi ya watendaji hao jambo ambalo linaleta usumbufu wakati inapoteka uchelewaji wa usafiri.

Dr. Mwita alizitaja changamoto nyengine kuwa ni uhaba wa Dawa, huduma
za umeme wa dharura, ongezeko la wagonjwa pamoja na utaalamu mdogo wa
watendaji wake kwa baadhi ya amashine za Kisasa zilizomo ndani ya Hospitali hiyo na kushairi kuandaliwa mpango maalum wa kupatiwa mafunzo.

Akizungumza na baadhi ya Madaktari na watendaji wa Hospitali hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Madaktari na Wauguzi wa Hospitali hiyo wanalazimika kuwajibika ipasavyo ili hadhi ya Hospitali hiyo iendelee kubakia.

Balozi Seif alisema mfumo huo wa uwajibikaji ulioambatana na vifaa vipya na vya kisasa unaweza kushawishi wagonjwa kutoka nje ya Visiwa vya Zanzibar kutaka kupatiwa huduma za Afya kwenye Hospitali hiyo ya Abdulla Mzee Mkoani.

Alielezea masikitiko yake kutokana na Hospitali nyingi nchini kulalamikiwa kutokana na huduma zake hawa wakiguswa zaidi Wauguzi kutokana na kauli zao za kuwavunja moyo wagonjwa wanaokwenda kutaka kupatiwa huduma za Afya.

Akizungumzia Makaazi ya Madaktari wa Hospitali hiyo Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshaamua kujenga nyumba Nne za Ghorofa kwa nia ya kuondosha tatizo
hilo.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeshazungumza na Kampuni iliyojenga Hospitali hiyo kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kujenga
Nyumba hizo ili kupunguza gharama za kumtafuta mkandarasi mwengine wa
ujenzi huo wakati utakapowadia.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika nasaha zake kwa watendaji
hao wa Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee Mkoani Pemba alisema Serikali isingependa kuona huduma za afya zinazotolewa kwenye Hositali
hiyo zinaambatana na ushabiki wa Kisiasa.

Balozi Seif alisema Hospitali ni sehemu ya huduma inayompasa mwananchi
ye yote mwenye matatizo ya kiafya anapatiwa huduma zinazostahiki bila
ya ubaguzi wala itikadi za kisiasa.

Alionya kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitamvumilia mtendaji ye yote wa Sekta ya Afya atakayeonekana ana tabia hiyo ya kushabikia masuala ya Kisiasa.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
301/2017.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashauri kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwanja hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli
Wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo
Wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya



 Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo

Habari picha na Mahmoud Ahmad,Monduli
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao

Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao .

Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.

“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti


Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.

Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.

Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .

“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare

Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia
You might also like: