Leo Februari 24,2016 ,Chama cha
Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club
International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa
madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi
Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza
changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana
wa Lions Club katika nchi ya Tanzania, Uganda na Sudani ya Kusini bwana
Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town...Madawati hayo 165
yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1
blog,Kadama Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho.
Gavana wa Lions Club International
katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo
mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata
wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha
Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge
Miongoni mwa madawati ya chuma 165
yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na
Mwenge katika manispaa ya Shinyanga
Hapa ni katika shule ya msingi Town
katika manispaa ya Shinyanga ,aliyesimama ni mwenyekiti wa bodi ya shule
hiyo Said Juma Issa akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliofika katika
shule wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 65 kwa shule hiyo na
100 katika shule ya msingi Mwenge
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Town wakiangalia madawati waliyopewa na Lions Club International
Kulia ni diwani wa kata ya Shinyanga
mjini,ambaye pia ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam
aliyefanya jitihada za kupatikana kwa madawati katika shule za kata
yake,Town na Mwenge.Diwani huyo pia ni mwanachama wa Lions Club International
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Town
Josephine Mabula akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro ambapo alisema shule hiyo yenye wanafunzi
1104 sasa haina uhaba tena wa madawati baada ya kupokea kutoka Lions Club International
Kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga Lewis Kalinjuna,katikati ni mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifuatiwa na gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Lewis Kalinjuna akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati,ambapo
mbali na kuipongeza Lions Club International
kwa kutoa msaada huo,aliwataka madiwani wa manispaa ya Shinyanga
kufanya kazi badala ya kukalia maneno maneno kwani kiongozi mzuri
anapimwa kwa maendeleo anayowaletea wananchi wake.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Lewis Kalinjuna alisema hivi sasa manispaa hiyo imeanza kutoa shilingi
milioni 10 kila mwezi kwa ajili ya kutatua changamoto ya uhaba wa
madawati katika shule za manispaa hiyo huku akiwataka wananchi kuendelea
kuisaidia serikali kwa michango mbalimbali ili watoto wasome vizuri
Gavana wa Lions Club International
katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema wameamua kutoa msaada huo
ili kuwaondolea changamoto wanafunzi ya kukaa chini wakati wa masomo ili
kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ikiwa ni moja ya majukumu yao
kusaidiaa jamii na serikali.Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi
kujenga moyo wa kutoa kwani serikali pekee haiwezi kumaliza matatizo ya
wananchi
Wanachama wa Lions Club International mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,ambao wameahidi kupaka rangi majengo ya shule ya msingi Town
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia kilichokuwa kinaendelea
Gavana wa Lions Club International
katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
akijiandaa kukata utepe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 165
kwa shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga
Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji tayari amekata utepe....
Gavana wa Lions Club International
katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
akishikana mkono na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada
kukabidhi madawati 165
Wanafurahia jambo.....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimshukuru Gavana waLions Club International
katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
kwa kutoa msaada wa madawati katika shule za manispaa ya
Shinyanga,ambapo alitangaza kujiunga na klabu hiyo ili kuungana na
wanachama wengine wa klabu hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliishukuru Lions Club International
kwa kuisaidia serikali kuchangia shule hizo huku akipongeza jitihada za
diwani wa kata hiyo kupigania shule zake kupata msaada huo wa madawati.
Matiro alitumia fursa hiyo kuwataka
madiwani wa manispaa ya Shinyanga kuiga mfano wa diwani wa kata ya
Shinyanga mjini Gulam Hafeez Mukadam ambaye amemaliza tatizo la uhaba wa
madawati katika shule za msingi katika kata yake huku akiwataka kufanya
kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuendekeza siasa na
maneno yasiyokuwa na faida kwa wananchi

Aliyesimama
ni katibu wa Lions Club ya Shinyanga bwana Sandip Lakhan akizungumza
katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.Alisema Lions Club ya mkoa wa
Shinyanga imetoa baiskeli kwa mkazi wa Bubiki wilayani Kishapu mkoani
Shinyanga Mussa Mipawa,ambaye ni mlemavu wa viungo,iliyotengenezwa na
mwanachama wa Klabu hiyo
Mussa Mipawa akiwashukuru wanachama wa Lions Club International kwa kumpa msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu

Bwana Mussa Mipawa akishikana mkono na mke wa Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
Bwana Mussa Mipawa akiwa katika baiskeli yake

Bwana Mussa Mipawa akiondoka na baiskeli yake-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni