Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kutokana na tabia ya baadhi ya
mgambo katika Halmashauri za Jijini la Dar es Salaam kujipatia fedha kwa
njia zisizo za halali, serikali kupitia Halmashauri zake imejipanga
kuwachukulia hatua za kisheria migambo wote watakaobainika
kujishirikisha na vitendo vya rushwa.
Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya
wanachi juu ya mgambo wanaochukua rushwa nje ya faini halali
zinazistahili kutozwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala,
Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shabibu amesema kuwa zipo baadhi
ya taarifa wamepewa na watawachukulia hatua kwa kuwasitishia mikataba
wale wote watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.
“ Wapo mgambo ambao watumia
vitambulisho feki na kufanya vitendo vya rushwa bado hatujawakamata ila
hatutawafumbia macho tutawachukulia hatua kali za kisheria kwa yoyote
atakayekamatwa akipokea rushwa na hata wale watakaotoa rushwa”
“Napenda kuwaasa watanzania
kuacha kuwapa fedha mgambo ili kukwepa kulipa faini halali hivyo basi
nawaasa watu kutii Sheria bila shuruti kama umefanya kosa kwa mujibu wa
Sheria lipa faini kwa mujibu wa Sheria lipa faini halali ili tuondoe
vitendo vya rushwa na kuiongezea mapato Serikali ”Alisema Tabu.
Afisa Tabu amewaomba watanzania
kutoa taarifa za mgambo wote wanaopokea rushwa na kusisitiza kuwa tabia
hii inayoendelea ikome mara moja na mgambo wote watakaobainika
kujihusisha na vitendo vya rushwa watasitishiwa mikataba yao ya kazi kwa
kukiuka maadili ya kazi zao
.
Mgambo katika Jiji la Dar es
Salaam wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuchukua rushwa kuanzia shilingi
5,000/= mpaka 10,000/= badala ya kutoza faini ya shilling 50,000/=
inayostahili kutoza kwa wale wanaokiuka kanuni na taratibu za afya na
mazingira katika Halmashauri mbalimbali.
Katika kupambana na suala la
mgambo wasio waadilifu,Halmashauri zimejipanga kuwaajiri vijana
walipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliopata mafunzo
yenye yenye kujenga uadili na uwajibikaji katika kazi ili kudhibiti
suala la mmomonyoko wa maadili na utendaji kazi mbovu wa mgambo katika
Halmashauri mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni