WAZIRI
 MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. 
milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye 
vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga,  wilaya ya Iringa vijijini 
mkoa wa Iringa.   Misaada
 hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo 
yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na 
kuwaacha wananchi wake bila makazi.   Akizungumza
 na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za 
mafuriko  na kuwapa pole wananchi hao leo mchana (Jumatatu, Februari 22,
 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia 
watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo. 
 
Wadau
 waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500,
 kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta
 ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni 
Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200  
vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-. 
 
Wengine
 ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na 
mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha 
kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 
vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya 
CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya
 saruji, kilo 100 za  maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali 
vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-. 
 
Madiwani
 wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum 
kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa 
wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa,  
Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/-
 ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa. 
 
Naye
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa 
Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni  20/- kati 
ya hizo sh. milioni  15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa 
Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bw. George Simbachawene.  Pia alikabidhi
 seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango 
kutoka Benki ya CRDB. 
 
Waziri
 Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 
250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 
1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati 
barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo.   Mapema,
 akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. 
Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua 
zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya 
nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza 
Februari 3, mwaka huu.   Alisema
 miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na 
kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao 
walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika 
na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao.   “Tangu
 Februari mosi, wamekkkwishapokea waginjwa wa kipindupinda 351 llakini 
walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu huyo wa mkoa.   (mwisho)   IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATATU, FEBRUARI 22, 2016.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni