NGOMA AFRICA BAND NA MZIMU WAO WA MZIKI WA DANSI ! WENYE MVUTO MKUBWA BARANI ULAYA


ngom1 ngom2 Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,ni bendi ya kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za washabiki huko ughaibuni.Bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake  katika kona zote duniani,pia imetajwa na vianzo vya habari vya kimataifa  kuwa  mdundo wa mziki wake umekuwa ni urimbo unao wanasa na kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani. Bendi ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU,Mtawala wa himaya ya Anunnaki Empire “ambaye  pia ndiye mtunzi,mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo,bendi yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao wakiwemo mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa solo gitaa ambae pia yupo katika safu ya uimbaji,Wengine ni  Matondo Benda,Aj Mbongo na Saidi Jazbo Vuai wapiga bass gitaa ,Jonathan Sousa aka “Jo Jo” (Drum),wapo akina dada FrolaWilliam,Jessica Oyah ,bendi hiyo maarufu ina wanamziki takriban kumi ,bendi hiyo pia imezungukwa na wataalamu .
Ngoma Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi mengi ya utani au usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina ambayo bendi hiyo haiwezi kuyakwepa !  Jina lingine ambalo lilikua gumu kwao kulikubali ni  “Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na baadhi ya wadau wa mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa  vitisho vya mbwa wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !
Ngoma Africa band imefanikiwa kufyatua CD nyingi ambazo nyimbo zilizomo katika santuri hizo zinatawala anga za redio za kimataifa..na kulitangaza kwa kasi kubwa jina la Tanzania kanji ya muziki , baadhi ya nyimbo zao ni pamoja “Rushwa ni adui wa haki” , Album “Mama Kimwaga”,Single CD “Apache wacha Pombe” , CD “Jakaya Kikwete 2010”,CD “Miaka 50 ya uhuru” na CD Bongo Tambarare na Uhuru wa habari, Single CD La Mgambo yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK, juzi kati waliachia singel CD mpya “Mapenzi Mpya” ambazo zote ni Utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU,mjeshi wa ambaye kufanya nae kazi inataka uwe na tabia za ki FFU, yaani uwe tayari tayari wakati wowote kwenda kutumbuiza hata ikiwa katika nchi za vita ! Na mdundo anautaka yeye lazima uwe na mwendo wa kasi na magitaa Lazima yalie milio ya kushambulia mashabiki katika ulingo wa dansi, mdundo ambao umepewa jina “Extra Ordinary” Bongo Dance mdundo ambao umefanikiwa kuwateka , kuwanasa na kuwatia kiwewe watu wengi katika kila kona duniani,
Wasikilize katika  website yao hapa www.ngoma-africa.com au pia http://www.itunes.apple.com/us/album/mama-kimwaga-sugar-mum/id947329929  ambayo mpenzi au mshabiki anaweza ku log in na kujumuika nao kama mwanachama wa bendi hiyo.
Ngoma Africa band inaonekana kuwa na mfumo tofauti sana ! Kuwa washabiki wanasauti kubwa ya kuweza kulazimisha maonyesho kuliko uongozi wa bendi !? Mashabiki mara nyingi wamekua tishio hadi kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho makubwa ya mziki…kama bendi ya Ngoma Africa haikualikwa au kupangwa katika ratiba ya onyesho
Fulani basi wapo tayari kususia onyesho hilo…au pengine wakalivunja !
Tena washabiki  hao wa umri wa lika na mataifa mbali mbali hawaoni wala hawasikii kitu kingine chochote mbele Bongo dansi la Ngoma Africa band aka FFU,ukipenda    waite  “Watoto wa Mbwa” au “Anunaki aliens” viumbe wa ajabu kutoka kutoka special Planet bongo land majina yote size yao !
Maporomota au waandaaji wa maonyesho mengi ya mziki huko ughaibuni wanalazimika Kuandaa  ulinzi wa kutosha mara tu wanapoialika bendi hiyo   kushiriki katika maonesho yao….hapa ndipo vianzo vingi vya habari vya ndani na nje  ya nchi vinapofika katangaza kuwa FFU wa Ngoma Africa band “jino kwa           jino” au “Jicho kwa Jicho” na washabiki .
 wasikilize katika tovuti yao www.ngoma-africa.com 
hapa http://www.itunes.apple.com/us/album/mama-kimwaga-sugar-mum/id947329929
pia unaweza kuwasiliana nao ka email hii
 contact@ngoma-africa.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni