Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Blogu ya Wananchi Media kesho itaadhimisha miaka mitatu tangu
kuanzishwa kwake, sherehe itakayofanyi Hyatt Regency Kempisky zamani
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa
blogu hiyo, Wiliam Malecela (Le Mutuz), alisema kuwa wameamua kufanya
sherehe kutokana na mafanikio waliyopata katika kipindi hicho, bendi ya
muziki wa kizazi kipya ya THT itatumbuiza.
Alisema licha ya kesho kufanya sherehe , leo itakuwa na semina maalumu
ya vijana 300, ambao watakuwa pamoja na matajiri 6 vijana na vijana
watatu viongozi wa wa kitaifa kwa lengo la kubadilishana
mawazo na matajiri na viongozi hao, ambao wataeleza walivyopigana mpaka
kufikia walipo kimaisha.
Alisema alianzisha blogu hiyo baada ya kuisajili kwa msajili wa
makampuni (Brela) 2012, ikianza kwa kutembelewa na watu 200 kwa siku
lakini kwa sasa inatembelewa na watu 70,000 mpaka 100,000 kwa siku kitu
ambacho anajivunia na kuwashukuru wadau.
Kampuni hiyo ilianza kwa mtaji wa dola ya Marekani 500, ikiwa na usajili
wa makampuni wa Brela, na inatoa ajira kwa vijana 4 waliomaliza vyuo
vikuu nchini na ina ofisi yake katika jengo la Tancot House Sokoine
Drive, Dar es Salaam.
Alisema katika miaka mitatu blogu imeweza kuwa na domain yake wenyewe ya www.williammalecela.com
na kuingia kwenyeFacebook, Twitter, na Instagram ambapo sasa
inarusha habari sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja na kuweza kuwafikia
watu hadi 500,000 kwa siku.
Alisema mipango ya baadaye ni kuwekeza kwenye kampuni mpya ya African Swahili Media Radio Television ambayo tayari
imeshapata leseni ya kufungua radio na televisheni ambayo inatazamiwa
kuwa hewani Aprili mwaka huu, kituo cha radio kitakuwa
Morogoro na televisheni Dar es Salaam, anatarajia kutoa ajira
zaidi angalau kwa vijana 10
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni