Mbunge wa 
Mafinga Vijijini, Cosato Chumi  (Mwenye diary mkononi) akipata maelekezo
 katika kiwanda cha kiwanda cha Sao Hill katika ziara ya kutembelea 
Taasisi Binafsi na za Umma. 
 Mbunge wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi (wa pili kutoka kushoto)akionyeshwa shughuli zinazofanywa katika kiwanda cha Sao Hill.
Wengine  ni Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu wa mbunge.
 Baadhi ya wafanyakazi wa sao hill wakiwa kazini.
 Sehemu ya nguzo zinazozalishwa  na kiwanda cha Sao Hill.
MBUNGE
 wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi amefanya ziara kutembelea  Taasisi za
 Umma na Binafsi kwa kutembelea Sao Hill Industries, Sao Hill Forest, 
Kiwanda cha Pareto na kampuni ya simu ya TTCL.
Katika
 ziara hiyo mbunge ametembelea Vituo vya Polisi, Taasisi ya Kuzuia na 
Kupambana na Rushwa (PCCB), NSSF , Bank za Mucoba, NMB na CEDB,Magereza 
,pamoja na Taasisi za Elimu.
Amesema kufanya ziara ni kujitambulisha, kufahamiana na kufahamu changamoto wanazokabiliana nazo.
Chumi 
amesema nguzo za umeme, kutoka Afrika Kusini  sio sahihi wakati 
 zinaweza kupatikana na uwezo wa kuzalisha  nguzo 90000 kwa mwaka.
Amesema
 kutokana na maelezo ya kiwanda hicho  na wamesema ikiwa watapata nafasi
 ya kuongezewa uwezo wa kuvuna kutoka Shamba la Taifa la Msitu wa Sao 
Hill, wanaweza kusambaza nguzo zaidi.
 Mgao 
wa kuvuna wa cubic 120,000 Changamoto ni kuwa wakipewa kitalu lakini 
ndani ya kitalu sio kila mti unafaa kwa nguzo kwa hiyo ombi lao, wapewe 
kwa mfumo wa kwamba wavune kile ambacho kinafaa kwa nguzo harafu miti 
inayofaa labda kwa karatasi ibaki kwa ajili ya Kiwanda cha mgololo.
wakati huohuo wawekezaji Mafinga waiomba Tanesco kuwafungia laini madhubuti ya Umeme katika kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni