VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI

Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.

Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.

Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.

“Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,

“Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).

Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.

Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.

Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa maelezo kuhusu YUNA inavyofanya kazi kwa jamii ya Tanzania na hususani vijana katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
IMG_3639
Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.
IMG_3508
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni