Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akiongea na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) 
alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa   ziara 
ya kuzitambua taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani 
akiongea  wakati wa kikao na wafanyakazi wa   Wakala wa Majengo 
Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, 
wakati wa  ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake  kushoto 
ni Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga.
Wafanyakazi wa   Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo 
katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika  ziara ya kuzitambua tasisi 
zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme 
(TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua 
tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu 
yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
(Kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa 
la Ujenzi (NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya 
kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu 
yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo 
katika picha) Mamilo  katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya 
wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo 
jinini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, amezitaka 
taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na kwa uharaka ili 
kuendana na kasi ya madiliko ya Serikali ya awamu ya Tano.
Ameyasema hayo jijini Dar  es salaam, wakati alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini 
ya Wizara yake ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Ufundi na 
Umeme (TEMESA) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)  kwa lengo la kupata mafunzo 
ya kiutendaji katika taasisi hizo.
Aidha amezitaka taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya 
mapato walivyonavyo na kamwe kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini.
“Nataka ifikapo mwaka wa fedha ujao makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi 
kuliko matumizi na kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka Serikalini, kikubwa ni kubuni 
vyanzo vyengine vya mapato ili kuweza kujiendesha”, alisema Naibu Waziri. 
Hata  hivyo Naibu Waziri huyo amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na 
bila woga kwani Serikali haitamuonea huruma yeyote anayekiuka kutekeleza wajibu 
wake.
“Nawaomba mfanye kazi kwa morali kubwa ili kuweza kuisaidia jamii ambayo inahitaji 
huduma muhimu kutoka Serikalini”, alifafanua Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA 
Eng. Manase Ole kujan kutatua changamoto walizonazo ili kuleta mabadiliko chanya 
katika taasisi hiyo.
“Una nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko hasa katika mfumo mzima wa ukatikatishaji 
tiketi eneo la Magogoni ambalo limekuwa kero katika mfumo mzima wa ukusanyaji wa 
mapato”, alisisitiza Naibu Waziri Ngonyani.
Sambamba na hilo Naibu Waziri amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo 
Tanzania  Arch. Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo itaonyesha idadi ya nyumba 
za Serikali wanazomiliki na ibainishe taarifa ya watumishi wenye stahili ya kupangishwa 
kwenye nyumba hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan 
amesema wakala huo umepanga kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini 
na kuhakikisha inapunguza  changamoto ya usafiri katika vivuko.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Eng. Julius Mamilo 
amebainisha changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa fedha hali inayosababisha 
Baraza hilo kukwama katika kufanya kazi katika miradi yake ya maendeleo hususan 
katika kufanya kazi za utafiti.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni