Wananchi
wa Eneo la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam wamelilalamikia Shirika la
TANESCO kushindwa kutatua Kero ya Nguzo ambayo inahatarisha Maisha ya
wakazi Hao katika eneo hilo kwa zaidi ya Miaka 8 hivi sasa, nguzo hiyo
imesogelea Kibanda cha Biashara na kusababisha hali ya Sinto fahamu
kufuatia usalama wao.
Wakizungumza
na Mtandao huu wakazi wa Eneo hilo wamedai yakuwa Taarifa walisha
peleka katika sehemu husika lakini Hadi leo hii ni mwaka wa Nane Bila ya
Mafanikio.
Mwaka
2008 wakazi hao waliiandikia Tanesco Barua ya kufanya Marekebisho ya
Kuomba Kuondoa Mstimu huo lakini hadi leo Mamlaka hiyo haijafanya hivyo,
Ila Mwaka 2015 mwishoni Tanesco ilifika eneo la tukio na kuangalia tu
na kuondoka bila ya kufanya Marekebisho yoyote.
Je
kwa hali hii Tunangojea Maafa au Hasara Itokee Ndio tukimbilie?
Tunaiomba Mamlaka Husika Iweze Kuchukua Hatua za Haraka kurekebisha hili
kabla ya Maafa hayajaweza Kutokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni