Juhudi
kubwa ya kufikisha elimu kwa jamii juu ya uhifadhi, usimamizi na
uvunaji endelevu wa misitu iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana na
mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia kampeni mbalimbali ikiwemo ya
mama misitu inayofadhiliwa na nchi ya Finland imeanza kuzaa matunda.
Baada vijiji kuanza kuhifadhi misitu, na wananchi kuunga mkono juhudi hizo baada yakuanza kunufaika na utunzaji huo.
Miongoni
mwa vijiji ambavyo wananchi wake wameanza kunufaika na uhifadhi wa
misitu ni kijiji cha Nanjirinji A, kilichopo wilayani Kilwa mkoani
Lindi.
Wananchi wa kijiji hicho wameanza kunufaika na mpango huo kupitia mapato ya uvunaji wa mazao ya msitu wao wa Mbumbila.
Mwenyekiti
wa serikali ya Kijiji hicho, Jafariri Nyambate alisema wameanza kutoa
ruzuku kwa akinamama wajawazito wakazi wa kijiji hicho. Kila mjamzito
hupewa shilingi 30,000 anapokaribia muda wake wakujifungua. Alisema.
Alisema
hilo nijambo moja kati ya mengi yaliyofanywa na kijiji hicho kwa
wananchi kutokana na mapato ya msitu waliohifadhi unaojulikanakwa jina
la Mbumbila.
Nyambate
ambaye kijiji chake pia kimeweza kuwanunulia sare wanafunzi wa shule ya
msingi ya kijiji hicho, kuchimba visima vya maji, kujenga soko la
kijiji, madarasa, nyumba ya mwalimu, kuweka umeme jua kwenye shule ya
kijiji hicho na kutoa ruzuku kwa akinamama wajawazito, alisema uenda
mafanikio hayo yasiwe endelevu.
Kutokana
na uvamizi wa wakulima na wavunaji haramu unatishia kurudisha nyuma
mafanikio hayo, kwani juhudi zakuwaondoa zimekuwa ngumu kufanikiwa
kwasababu wakulima wamekuwa wakirejea kila unapofika msimu wa kilimo wa
zao la ufuta.
"Wanatumia
nguvu kulima ndani ya msitu na wanapambana na kamati yetu ya maliasili
inapofanya doria, mara moja wamewahi kuwazidi nguvu walinzi wetu na
kupora pikipiki," alisema Nyambate.
Kuhusu
uvunaji haramu, Nyambate alisema wakulima na wavunaji haramu wengi
wanatoka nje yakijiji na wilaya hiyo, akibainisha kwamba kuna mahusiano
na ushirikiano mkubwa kati ya wakulima wavamizi na wavunaji haramu.
"Wakulima
wengi wanaishi kwenye misitu ya hifadhi ya wazi ambayo inapakana na
msitu wetu, wanawaongoza wavunaji haramu ambao mazao ya msitu wanayoiba
wanahifadhi ndani ya vibanda vya wakulima hao,"alisema Nyambate.
Ofisa
mtendaji kata wa kata ya Nanjirinji, Haji Limba, alikiri kuwa mapato
yanayotokana na msitu huo yamesababisha kuanza kuwa na uhakika wa ulinzi
kwenye kata hiyo iwapo ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa
katika kata hiyo kitakamilika.
Alisema
sehemu ya fedha zinazotumika katika ujenzi huo zilichangwa na kijiji
hicho ambazo zilitokana na mauzo ya mazao ya msitu wa kijiji hicho.
Hata hivyo alibainisha kwamba wakulima wa ufuta na wavunaji haramu wnatishia kukwamisha mafanikio yaliyoanza kufikiwa.
"Hata
hivyo juhudi kubwa inayofanywa na uongozi wa kijiji,kata,halmashauri ya
wilaya na mkuu wa wilaya ya Kilwa zinapunguza kasi ya uvamizi wa
wakulima hao na wavunaji haramu,maana msaada kutoka wilayani ni mkubwa
sana,"alisema Limba.
Naye
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ngunichile wilayani Nachingwea,
Seif Ng'wang'wa ambaye kijiji cha kimehifadhi msitu wenye ukubwa wa
hekta 1296 unaojulikana kwa jina la Namitonga, alisema wavunaji haramu
baada ya kumaliza miti katika misitu ya wazi ya vijiji jirani na kijiji
hicho, wameanza kuvamia msitu huo.
Alisema kazi ya kuulinda imekuwa ngumu baada ya wavamizi kubadili mbinu.
"Tunajitahidi
sana kufanya doria mchana, walipogundua kuwa mchana inawawia vigumu
kufanya uhalifu wanafanya usiku,"Alibainisha kuwa uharibifu unaofanywa
na wavunaji haramu unatishia kufikiwa na kutekelezwa mipango ya
maendeleo ambayo utekelezaji wake ulitegemea mapato ya mauzo ya mazao ya
msitu huo.
Ofisa
mtendaji wa kijiji hicho, Seleman Soya alisema licha ya wavunaji haramu
lakini pia changamoto nyingine niwakulima kuvamia msitu huo.
"wavamizi
niwengi nivugumu sisi wenyewe kukabiliana nao, watatushinda nguvu
inahitajika nguvu kubwa kutoka serikalini vinginevyo watazidi
kuumega,"alisema na kutahadharisha Soya.
Alisema
migogoro ya mipaka baina ya vijiji hasa ambavyo havija hifadhi misitu
inachangia kukwamisha wananchi kukosa matumaini ya kunufaika na msitu
huo.
Bibi
Arafa Batazari(80) mwananchi wa kijiji hicho, alisema licha ya wananchi
kutarajia kunufaika na mauzo ya mazao ya msitu huo, lakini pia hali ya
ukame inaweza kurejea katika maeneo hayo.
Anasema tangu waanze kuhifadhi misitu, ukame ulianza kupungua kutokana na mvua kunyesha mara kwa mara.
"Tulianza
kupata mvua kama zamani, maana mito na vijito vilikuwa vinataririsha
maji muda wote kwa sababu kulikuwa na miti kandokando ya mito na
vijito"lakini wakulima walifyeka miti yote ikawa haitunzi wala
haitirirish maji tena mvua ikaanza kuadimika,"alisema bibi huyo.
Tatizo
hilo lipo pia katika kijiji cha Miima, wilaya ya Lindi. Kaimu
mwenyekiti wa kijiji hicho ambacho kimehifadhi msitu wenye ukubwa wa
hekta 2262, Omari Katenda, alisema uvunaji haramu kwa kutumia misumeno
ya moto umeshika kasi na kutishia uwepo wa msitu huo.
Alisema hali ya msitu huo ni mbaya, aki taadhirisha zisipochukuliwa hatua za haraka kudhibiti kasi hiyo unaweza kutoweka.
Alisema
baadhi ya wavunaji ambao leseni zao zinawaruhusu kuvuna kwenye misitu
ya wazi wanavuna kwenye msitu huo bila kufuata taratibu na kwakutumia
misumeno ya moto.
Mwenyekiti
huyo ambae anakaimu baada ya viongozi wa awali wa kijiji hicho
kuondolewa na wananchi kutokana na tuhuma ya kushindwa kudhibiti uvunaji
haramu na kushirikiana na wavunaji hao.
Alisema
hivi sasa wavunaji haramu wanapitia vijiji jirani ambavyo havija
hifadhi misitu na kudai maeneo wanayovuna yapo nje ya kijiji na msitu
huo.
Aldophina
Mbwago, mjumbe wa serikali ya kijiji hicho alisema uvunaji haramu
unashamiri kutokana na kiwango cha adhabu wanachoadhibiwa wavunaji
haramu.
Alisema udhaifu wa sheria uliopo unatumiwa na wavunaji kukiuka taratibu, kanuni na sheria.
"Wavunaji
wanakutwa wametumia misumeno ya moto wanatozwa faini ya shilingi ya
shilingi1,000,000 ambayo nikidogo ikilinganishwa na hasara na madhara
yatayotokea baada ya nchi kugeuka kuwa jangwa,"Alishauri kosa la uvunaji
haramu na kutumia misumeno ya moto liingizwe kwenye makosa ya uhujumu
uchumi.
Tatizo
hilo lipo pia katika kijiji cha Kiwawa katika wilaya hiyo ya Lindi.
Diwani wa kata ya Kiwawa, Mohamed Mkulyuta, alisema msitu uliohifadhiwa
na kijiji wenye ukubwa wa hekta 8896, upo katika hatari ya kutoweka
kutokana na kasi ya uvunaji haramu unaofanyika.
Akibainisha
kuwa mgogoro wa mipaka baina ya kijiji hicho na vijiji vya Namkongo na
Mputwa unachangia kushamiri kwa uvunaji huo kwasababu wavunaji na
wakulima wanasema maeneo wanayovuna na kulima yapo kwenye vijiji vya
Namkongo na Mputwa.
Ahmad
Tendele, mwananchi wa kijiji hicho, alisema msitu huo upokatika hatari
ya kutoweka kutokana na kasi ya uvunaji haramu iliyopo kwenye msitu
huo.
"Hali
nimbaya sana kwenye msitu,lakini mgogoro wa mipaka kati ya kijiji na
Mputwa na Mkongo unachangia uharibifu huu, na mpaka sasa hatujui
serikali itamaliza lini mgogoro huu,"alisema Tendele.
Baadhi
ya viongozi na watendaji wa wilaya wamekiri kuwepo kwa tatizo
hilo, huku wakieleza mikakati yao katika kudhibiti na kukomesha tatizo
hilo.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Oliver Vavunge alikiri kuwa
tatizo la wavunaji haramu lipo pia katika vijiji vya halmashauri hiyo.
Alisema
kwa kutambua uzito wa tatizo hilo, halmashauri yake imetengeneza kikosi
kazi kinachoundwa na watalamu kutoka katika idara mbalimbali za
halmashauri hiyo.
Timu
ambayo inafanya doria kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji na kata
inazotembelewa na timu hiyo, ambayo hupeleka taarifa zinazoelezea
mafanikio na changamoto ya doria hizo kila wiki.
Alisema
taarifa hizo husomwa na kuwekwa hadharani kila mwezi. Mkuu wa wilaya
ya Lindi, Yahaya Nawanda, alisema anatambua umuhimu wa kuhifadhi na
kuendeleza misitu.
Hivyo
wamejipanga kukabiliana na wavunaji haramu na wakulima wanaovamia
misitu ya hifadhi. Akionya kuwa kutakuwa na doria za mara kwa mara tena
za kushitukiza, hata hivyo hakutakuwa na upendeleo wala ubaguzi kwa wale
wote watakaokamatwa kupitia doria hizo au njia nyingine.
"Msako
utakaofanyika hauta angalia cheo, hadhi wala madaraka ya mtu ambaye
atabainika kutenda vitendo hivyo au kushiriki kufanikisha vitendo hivyo,
maana kama sisi tumerithi misitu lazima jitihada zifanyike ili nasi
turithishe kwa vizazi vijavyo," alisema Nawanda.
Kwa
upande wake, mkuu wa idara ya ardhi na maliasili wa halmashauri ya
Wilaya ya Nachingwea, Lington Nzunda. Akizungungumzi kwa niaba ya
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, alisema halmashauri inamikakati
na mipango mingi ya kuhakikisha kasi ya uvamizi wa misitu na uvunaji
haramu unapungua kama siyo kwisha kabisa.
Miongoni
mwa mipango aliyoisema na kuitaja ni pamoja na kuvihamasisha vijiji na
kuviwezesha ili viingie kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Akibainisha
kuwa wananchi wakianza kuona faida ya kuhifadhi misitu, watakuwa
walinzi wazuri wa misitu hiyo na kuongeza kusema;"Wananchi wanawatambua
wavunaji na waharibifu wengine wa misitu kwa sababu wengine wanaishi
nao, lakini hawawafichui ,"alisema Nzunda.
Aliutaja
mkakati mwingine ambao umeanza kutekelezwa ni Halmashauri hiyo kutoa
mafunzo kwa askari wa vijiji, ambao watakuwa wanashirikiana na kamati za
maliasili za vijiji kufanya doria kwenye Misitu yote iliyo kwenye
maeneo ya vijiji.
Uenda
tatizo la uharibifu wa misitu halipo katika vijiji hivyo tu hapa
nchini. Unaposikiliza maelezo ya wananchi na viongozi wa vijiji
unagundua kuwa baadhi ya wananchi wameanza kutambua faida za kuhifadhi
misitu na hasara zinazotokana na uharibifu wa misitu.
Kwa
upande mwingine mipango na mikakati ya serikali katika kudhibiti na
kukabiliana na uharibifu wa misitu. Jambo lililomuhimu kwetu wote
nikusaidia mapambano hayo kwa nafasi zetu. Kwani madhara ya uharibufu
huo hayataishia kwa wananchi wa vijiji hivyo wala kwa watendaji na
viongozi wa serikali, bali kwetu sote. MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni