
picha kwa hisani ya  maktaba
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Mkuu
 wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji 
katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa 
kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo 
ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza 
kuhatarisha uhai wa maisha yao.
Katika
 kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo 
ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka 
yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa 
inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani 
waliendelea na shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha
 Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na 
yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa 
kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba 
kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.
Alisema
 kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo
 linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .
 Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias
 Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya 
mkuu wa wilaya  ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala  ambapo alisema 
kuwa pia iatawasaidia  kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na 
uchimbaji holela.
Aidha
 pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano
 ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa 
mwezi mmoja .
Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao  ambapo walisema kuwa hawakubaliani
 na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya
 kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali 
iangalie namna nyingine.
"kwakweli
 tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi
 ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula 
,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha 
yetu"Alisema Lowayani Metili
 Ipo
 haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na 
serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati 
wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga 
wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni