Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha 
Nandagala wilayani Ruangwa ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya 
HUAWEI ya China , kijijini hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu 
wa Mkoa wa Lindi, Jordan Lugimbana.
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka 
kwa Mtalaam wa Ufundi wa Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, 
Tran The Hoang ili ziweze kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa 
baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa 
katika ziara ya siku moja wilayani humo Februari 29, 2016.
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ma  Mwanaidi Mussa  na Mkussa Lukoloma 
(kushoto) wote wa kijiji cha Nandagala wilayani  Ruangwabaada ya 
kuwakabidhi kadi zao za bima ya Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya 
Simu ya Halotel iliyochangia shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa
 kijiji hicho kufaidi huduma za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. 
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa 
Mwenyekiti  watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua 
katika kijiji cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda
 kijijini hapo kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. 
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Ruangwa baada ya 
kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28, 2016. (Picha na 
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni