  | 
| 
 
Mkurugenzi
 wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati 
kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  
na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya 
millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za 
Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana  
 | 
  | 
| 
 
Mkurugenzi
 wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro
  kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja  
na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya 
millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za 
Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana  
 | 
  | 
| Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa
 pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye 
thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika 
kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana . | 
Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa
 pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye 
thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika 
kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
  | 
Mkurugenzi
 wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na waandishi wa 
habari mara baada ya kukabidhi misaada kwa  Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh 
Amina Masenza (kushoto) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa 
vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia 
zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani 
Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana . 
………………………………………………………………………………………………… 
 Iringa,
 Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye
 thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa. 
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida. 
“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa
 pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na mashuka 35. 
Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba
 zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza. 
Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango
 wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka. 
 
 | 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni