NAIBU
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. 
Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la 
Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa 
kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia
 husika.
Dk.
 Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya 
Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili 
wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo
 mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha 
muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.
Aidha,
 Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza 
kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi
 na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.
Kwa
 upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, 
dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na 
pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia 
kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka 
kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n 
ahata kumsababishia matatizo.
Duka
 hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni 
miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha
 wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile
 inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka 
huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango
 hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.
Dk.
 Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni 
la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa 
taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia 
atachukuliwa hatua stahiki.
Tazama  tv, Kuona video hiyo hapa: 
Imeandaliwa na Andrew Chal.
(Picha zote na Andrew Chale.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni