MZEE KASSIM MAPILI AFARIKI DUNIA

Mzee mapili
Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania Mzee Kassim Mapili hatunae tena, amefariki dunia. 

Taarifa za kifo chake zinasema kwamba Mzee Mapili aliingia chumbani kwake jumanne usiku akitokea kuangalia mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Arsenal na Barcelona, na toka alipoingia hakutoka tena, hivyo jioni ya jana alhamisi majirani walilazimika kutoa taarifa ambapo polisi walivunja mlango wa chumba chake na kumkuta amefariki.

Tutawaletea taarifa zaidi.Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni