Mkurugenzi
wa Mipango miji na Vijiji Zanzibar Dkt. Mohammed Juma akizungumza kando
ya Warsha ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya
Zanzibar huko Shangani mjini Zanzibar.
Mwezeshaji
wa mafunzo kutoka Taasisi ya Mazingira ya Finland Bi Riihz Teinirants
akielezea hatua mbalimbali za kufuatwa kwa maafisa mbalimbali
walioshiriki mafunzo ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na
mazingira ya Zanzibar huko Shangani mjini Zanzibar.
Picha
no - 0707 na 0710 Baadhi ya Maafisa kutoka Zanzibar na wenzao wa
Finland wakijadiliana namna ya bora ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa
Maeneo na mazingira ya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru
Shangani mjini Zanzibar.
Picha
no - 0687 Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali za Zanzibar wakisikiliza
mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Maafisa kutoka Finland juu namna ya
bora ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya Zanzibar
katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru Shangani mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
IDARA
ya Mipango miji na Vijiji Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi
mbalimbali za Zanzibar wanatarajia kuanzisha Kituo cha Mtandao wa
Taarifa za Maeneo na mazingira ya Zanzibar ambapo Wananchi watalazimika
kupata taarifa kupitia kituo hicho.
Taarifa
hizo zitawekwa katika mfumo wa kidigitali na kuwekwa katika Mtandao huo
ili kuepusha upotoshaji wa taarifa na pia zipatikane kwa wakati bila ya
usumbufu.
Mkurugenzi
wa Mipango miji na Vijiji Zanzibar Dkt. Mohammed Juma ameyasema hayo
wakati wa warsha ya kuandaa utaratibu wa kuanzisha kituo hicho cha
Mtandao Shangani mjini Zanzibar.
Amefahamisha
kuwa kutokana na kuwepo kwa Vyanzo vingi vya Taarifa zinazohusu Maeneo
ya Zanzibar kunapelekea baadhi ya Taarifa hizo kutokuwa sahihi na
kupelekea mkanyiko katika jamii.
“Kwa
sasa kuna Vyanzo vingi vya kujua maeneo na mazingira ya Zanzibar..kwa
mfano ukienda kutaka taarifa juu ya eneo fulani inawezekana taarifa hiyo
ikatofautiana na Vyanzo vingine lakini tutakapokuwa na Chanzo kimoja
taarifa zitakuwa moja na sahihi”Alisema Dkt Mohamed.
Ametaja
faida zitakazopatikana kupitia Mtandao huo kuwa nipamoja na
kuwarahisishia Wananchi kupata taarifa popote walipo na kwa wakati
kinyume na ilivyo sasa ambapo hulazimka kwenda katika Taaisi husika
jambo ambalo huwaletea usumbufu.
Aidha
amesema pia itakuwa ni sehemu ya uwazi kwa Serikali kupitia Taasisi
zake ambapo kila kitu kitawekwa wazi na kupatikana kirahisi kupitia
Mtandao huo.
“Mtandao
huo utaweka wazi maeneo yote yakiwemo,Makaazi,maeneo ya
uwekezaji..isipokuwa yale yakiusalama ili kumrahisishia mwananchi kuweza
kupata Taarifa bila kuhangaishwa huku na kule” alibainisha Dkt
Mohammed.
Aidha
amebainisha kuwa katika Warsha ya kuandaa Mtandao huo Taasisi nane
zimeshiriki ili kuwa na sauti moja juu ya maeneo na mazingira ya
Zanzibar.
Amezitaja
taasisi hizo kuwa ni pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa ardhi, Idara ya
Mazingira, Idara ya Misitu na maliasili zisizorejesheka na idara ya
maendeleo ya uvuvi.
Taasisi
zingine ni pamoja na Idara ya Rasilimali za baharini, Chuo kikuu cha
taifa SUZA na Mamlaka ya Mazingira Zanzibar (ZEMA) ambazo zote
zimeshiriki katika Mpango huo wa kuandaa Taarifa za pamoja.
Jumla ya shilingi Milion 140 zitatumika kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao ambazo ni msaada kutoka Serikali ya Finland.
Kwa
upande wake Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Taasisi ya Mazingira ya
Finland Bi Riihz Teinirants amesema Taasisi watendaji wa Taasisi hizo
walioshiriki mafunzo wanajukumu la kuwafahamisha wenzao ili kutimiza
lengo lililokusudiwa.
Aidha
bi Riihz amesema mbali na kutoa mafunzo ya kuanzisha Kituo hicho cha
Mtandao wataisaidia Zanzibar kutafuta taarifa za maeneo yake na kuziweka
katika Kituo hicho hasa zile za mwambao wa bahari ili kuleta ufanisi
unaohitajika.
Kunzishwa
kwa kituo hicho cha Mtandao wa Taarifa za maeneo ya Zanzibar ni matokeo
ya kukamilika kwa Mradi wa kutunza mazingira Zanzibar (SMOLE)
uliofadhiliwa na Serikali ya Finland katika kuisaidia Zanzibar ambapo
Mradi huo ulipata mafanikio makubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni