Na Dixon Busagaga wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi
mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na
matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia
silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni
mwa mwaka huu.
Mbali na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
“
Wakati
huo huo matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto
yameendelea kushika kasi mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja
(jina limehifadhiwa ) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua
katika jaribio la kubakwa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold Josephate ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.
Alisema
tukio jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo
mwanamke mmoja aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya
kunyongwa shingo.
“
Alisema eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo .Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni