UVCCM ARUMERU WALAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA MKOA KUMSIMAMISHA KAMANDA WAO



  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya
baadhi  ya  wajumbe waliouzuria mkutano huo
  Na Mahmoud Ahmad,Arusha
BARAZA la Umoja  wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) wilaya ya
Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa
umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na
kuisaliti CCM  katika uchaguzi mkuu wa mwa Oktaba 25 mwaka jana.
  Aida baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha,  Lengai  Sabaya na kumtaka ajitathmini
na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona
hawezi ajing'oe mwenyewe.
  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,aliesema kuwa
wanamtambua  Manga ambaye pia ni  mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa
(NEC),kama Kamanda wao wa vijana.
  "Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza la tumetathmini
tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka
yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya
kukijenga"alisema na kuongeza
  "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa
kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe
mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa
dhidi ya kamanda wetu"
  Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na  kumtaka Manga
asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe
nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.
  Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao
alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
kutoka nje.
  Naye Anjelina Lukumay ambaye ni mjumbe wa baraza hilo kutoka Kata ya
Oldonyosambu,alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa,Lekule Laizer
kuliangalia suala hilo na kulitafutia ufumbuzi kwani Sabaya amekiuka kanuni
za chama.
  "Mwenyekiti wa wilaya ametumia kanuni ipi kumkataa kamanda wetu bila
kutushirikisha?hatutakubali kuvurugwa wilaya ya Arumeru,tumepokea kwa
mfadhaiko kauli hiyo kwani Sabaya kachaguliwa hata miezi miwili hana ila
inakuwaje anataka kumtoa Manga tena bila kutushirikisha?alihoji Anjelina
  Wiki iliyopita uamuzi wa kumsimamisha Manga ulifikiwa katika  kikao cha
baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kilichozinduliwa na kaimu katibu mkuu Shaka
Hamdu Shaka,ambapo kikao hicho kilikuwa na wajumbe 34 huku 33 kati yao
wakipiga kura za ndiyo.
  Pia kikao hicho kilitoa onyo kali kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Arusha
Mjini,Longido na Monduli na kuwataka wajipime na kujitathimini kama
wanatosha kuwa makamanda wa UVCCM na  wakiona hawatoshi tunaomba wakae
pembeni kabla  baraza halijawachukulia hatua.
  Uamuzi wa kumsimamisha Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya
taifa (NEC)wilaya ya Arumeru   ulifikiwa katika Manga
Akisoma tamko lilitolewa na Kikao hicho cha baraza  kikao hicho cha
baraza Katibu wa Hamasa wa (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lucas Nsomi alisema
Manga kuanzia wakati huo  si kamanda wa Vijana Wilaya ya Arumeru tena kwani
amepoteza sifa baada ya kudhibitika kukisaliti chama kwenye uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015,kwani wakati wa uchaguzi huo alionekana akifanya vikao
vyakufanikisha ushindi kwa UKAWA.
  “Kikubwa alichofanikiwa Manga ni kuwagawa vijana wa Arumeru hali
inayopelekea kushindwa kuijenga jumuiya hiyo na kuanzia sasa sio kamanda wa
vijana tena wa wialaya hiyo na sipo tayari kufanya naye kazi yoyote ile
ndani ya CCM”.
  Sabaya  alidai kuwa vijana waliompitisha kuwa kamanda lilikuwa ni genge
la wahuni ambao walikuwa wakiendesha vikao vya vijana wenye njaa na kuwa
hayupo tayari kuwa Mwenyekiti wa magenge ya vijana wenye njaa na wasaliti
ndani ya CCM.

SERIKALI YAOMBWA KUTENGA FEDHA KILA MWAKA KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE KONGWE YA ILBORU

 
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga fedha za ukarabati kila mwaka kwa shule
kongwe ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Ilboru   ili walau kuzirudisha
katika hali yake nzuri na kuzijengea mazingira mazuri ya kujifunzia na
kufundishia, ili zionekane tofauti na shule zingine hatimaye ziwafanye
wanafunzi  wajitume zaidi katika masomo.

Hayo yalisemwa  jana na mkuu wa shule kongwe  ya Ilboru  sekondari  Julius
Shulla alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu  na walezi katika mahafali
ya 24 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.

Alisema kuwa shule hiyo kongwe na ambayo imekuwa ikitoa wataalamu mbali
mbali imekuwa ina uhitaji wa kukarabatiwa na hivyo ili kuondokana na hali
hiyo serikali inapaswa kutenga fedha kila mwaka ili kuweza kuirejesha shule
hiyo katika mazingira mazuri yatakayowavutia wanafunzi.

Alileleza kuwa shule hiyo inakabiliwa  na changamoto ya uchakavu mkubwa wa
madarasa na nyumba za watumishi hali ambayo inasababisha mara nyingi
wanafunzi kukosa mahala pazuri pa kujifunzia hivyo kuwakatisha tama
kimasomo.

“tunaiomba na kuishauri serikali yetu sikivu iendelee kutenga fedha za
ukarabati kila mwaka kwa shule hizi kongwe ili kuzirudisha katika mazingira
yake mazuri ikizingatiwa hii ni shule ya wanafunzi wenye vipaji maalum
kiakili hali hii itawafnya wanafunzi wajitume zaidi katika masomo kwa kuwa
na mazingi mazuri ya kujifunzia”aliongeza Shulla.

Aidha Shulla alitaja changamoto  zingine zinazoikabili shule hiyo kongwe
kuwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo
hali hiyo inatokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi
ikilinganishwa na idadi ya walimu.

Alifafanua kuwa tatizo hilo husababisha shule hiyo kutafuta walimu wa muda
wa masomo ya Fizikia,kemia ,na hisabati ambao malipo yao ni makubwa sana
kwa mwezi ambapo shule haina uwezo wa kumudu gharama hizo kila mwezi.

Aliwataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata katika kutatua matatizo
yao na matatizo ya jamii yote kwa kufuata sheria na taratibu za nchi huku
wakijiepusha na uzembe ,ulevi,uvutaji bangi na matumiz ya madawa ya kulevya
kwani hivyo vyote havina tija katika maendeleo.

HOSPITALI YA TENGERU YAKABILIWA NA UHABA WA VITANDA


 picha ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi  msaada wa vyandalua
 wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo
 mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja  na watoto wawili  wakiwa kila mmoja ana mama yake

Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Hospitali ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiliwa na ukosefu wa
vitanda hali ambayo inapelekea  wagonjwa kulala zaidi ya  mmoja katika
 kitanda kimoja.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  hili wagonjwa  hao mara baada ya kupokea msaada
wa vyandalua  kutoka kwa wafanyakazi  wa mfuko wa hifadhi ya jamii
(NSSF) tawi la Arusha walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali
hiyo wamekuwa wanapata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa
kwani wana banana sana na wakati mwingine wanakosa kabisa vitanda.
Mmoja wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo
alisema kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo
inawafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika vitanda
hivyo vichache
Unajua mfano mimi nimekuja hapa unaniona nipo na mtoto wangu lakini
tunalala wawili kwaiyo ukichanganya na watoto wetu maana unaona hii ni
wodi ya mama na mtoto tunakuwa wanne kweli tunaomba sana serekali
ituangalie sana hospitali hii kwani tunateseka nasio kuteseka tu sasa
tunavyobanana hivi muda mungine tunaweza ata kutoka na magonjwa
mengine  umu,unakutwa umemleta labda mtoto anaumwa ugonjwa huu tukija
apa huku kubanana badala ya kupona anatoka na gonjwa lingine kweli
watuangalie sana”alisema Lea Mmari
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali hiyo ya wilaya  ya Tengeru
Ukio Kusirigwa alisema kuwa ni kweli tatizo la vitanda lipo lakini sio
kubwa kikubwa kinachowakabili hospitali hiyo ni kukosekana kwa wodi za
kuwalaza wagonjwa hali ambayo inawafanya wawabananishe katika vitanda
hivyo.
“unajua siwezi sema kuwa tatizo la ukosefu wa vitanda hamna hapana
lakini shida kubwa ata tukipata vitanda sasa ivi tutaviweka wapi na
wodi zimeja ,hospitali hii ya wilaya imekuwa inapokea wagonjwa wengi
kutoka tengeru hapa ,mererani  na ata kia na kikatiti maana hii ndio
hospitali kubwa ya wilaya iliopo karibu hivyo kwa wingi huo na
ukiangalia wodi ni chache tunakosa jinsi hivyo inatubidi  wagonjwa
walale wawili wawili ili waweze kupata huduma”alisema Kusirigwa.
Aidha aliwaomba wadau pamoja na serekali kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi kama vile wafanyakazi wa NSSF tawi la Arusha walivyojitokeza
kuja kutoa misaada angalau ya vitanda,majengo  na kikubwa zaidi
aliwaomba sana waisaidie hospitali hiyo kujenga wodi kwa ajili ya
wagonjwa wakiwemo wakina mama na mtoto.
Naye meneja wa NSSF Frank Maduga alisema kuwa wao kama wafanyakazi
wameamua kujichanga na kuweza kusaidia hospitali hii kwa kuwapa
vyandalua hii ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa
malaria.
Alisema kuwa mpaka sasa wameshatoa vyandarua 184 katika hospitali
tofauti ikiwemo ya Mount meru ,St Elizabeth,Levolosi  pamoja na kwenye
vituo vya kulelea watoto yatima na wasiojiweza ambacho ni kituo cha
walemavu  Usa river na hawataishi hapo tu wao kama wafanyakazi
wamejipanga kila mwisho wa mwezi kutoa msaada  katika kila sehemu
ambayo inamlenga mwananchi.
Alitoa kwa wadau mbalimbali  kujitoa kwa kuchangia na kusaidia kwa
kutoa misaada katika sehemu mbalimbali ikiwemo watoto yatima ,wasio
jiweza na hata katika hospitali zetu ili kuweza kuwapa moyo wahusika
na sio kusubiri tu serekali ifanye ,kwani kutoa ni moyo ivyo kila mtu
anaeguswa ajitokeze kutoa ikiwemo kuchangia wodi za hospitali hiyo.

DC SIMANJIRO AWAPA WIKI MOJA WAJUMBE WA SEREKALI YA KIJIJI KURUDI OFISINI LA SIVYO UTAFANYIKA UCHAGUZI MWINGINE WA VIONGOZI


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Lucas Mweri akisoma mapendekezo mbalimbali kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi (kushoto) ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck.
Na Mahmoud Ahmad,Simanjiro

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Mahmoud Kambona ametoa wiki moja kwa wajumbe 12 wa Serikali ya Kijiji cha Kambi ya Chokaa waliosusa kutumikia nafasi hiyo kurejea ofisini au uchaguzi mwingine ufanyike.

Inadaiwa kuwa wajumbe hao walisusa kufanya kazi wakipinga kuchaguliwa Mwenyekiti Mbuki Mollel badala ya Joshua Kuney, hivyo shughuli za utawala kwenye kijiji hicho zinashindwa kufanyika kutokana na kutokuwepo uongozi.

Kambona alitoa agizo hilo juzi mbele ya baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kwani michango na huduma za kijamii hazifanyiki na kiongozi aliyepo ni mtendaji wa kijiji pekee tangu mwaka juzi uchaguzi ulipofanyika.

Alisema anawapa muda wa wiki moja viongozi hao warudi ofisini na endapo hawatakubaliana na hali hiyo uchaguzi ufanyike upya kujaza nafasi hizo il ishughuli za kiutawala wa kijiji hicho ziendelee kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri alibainisha vyanzo vya mapato vinavyotarajiwa kukusanywa na halmashauri ambavyo awali vilikuwa vinakusanywa na vijiji.

“Vyanzo vya ushuru wa mchanga, kuni kavu na samaki wakavu, ambavyo awali vilikuwa vinakusanywa na vijiji, hivi sasa vitakusanywa na halmashauri kisha itatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya vijiji husika,” alisema Mweri.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Jackson Sipitieck, alisema makusanyo na ushuru unapaswa kufanywa na halmashauri, kisha inarudisha kwa jamii kutokana na kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Huko vijijini ndipo kunaliwa fedha za ushuru na michango mbalimbali, hivyo halmashauri itakusanya na kurudisha kwa kujenga shule, barabara, zahanati na kuibua miradi mingine ya maendeleo kama inavyofanya,” alisema Sipitieck.

MARIA STOPES YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA JIJI LA MWANZA NA DAR JUU YA UZAZI WA MPANGO


Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi ya Health Promotion Tanzania (HPT), Bw. James Mlali akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Mwandishi wa wandishi na Muandaaji wa vipindi wa habari wa Redio Free Afrika ya Mwanza, Migongo akiuliza swali kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Wasimamizi wa Mafunzo hayo kutoka Maria Stopes Tanzania.
Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Bi. Shida Masumbi akiwaonyesha waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam moja ya njia mojawapo inayotumika katika uzazi wa mpango.
Mhadhiri wa SJMC- UDSM, Bw. Abdallah Katunzi akitoa mwongozo kwa waandishi wa habari juu ya mafunzo waliyoyapata waweze kuyafanyia kazi ipasavyo.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Citizen, Bernard Lugongo akiuliza maswali. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – Mwanza.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Cathbert Angelo Kajuna, Mwanza.
 
ASASI ya Health Promotion Tanzania (HPT) inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango imeiomba Serikali kuongeza bajeti ya uzazi wa mpango ifikie Sh. bilioni sita.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi hiyo, James Mlali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuhusu ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango.
 
Alisema asilimia 27 ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na asilimia 25 wanakosa huduma hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa na Serikali.
 
Mlali alisema bajeti ikiwa ndogo hata elimu inakuwa ndogo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.
 
“Bajeti inayotengwa inatakiwa iendane na ongezeko la idadi ya watu kwa kuzingatia upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni elimu,afya, na ajira.
 
“Pia ongezeko hili alizingatie hali ya uchumi kwasababu asilimia 42 ya watoto wamedumaa akili kutokana na ukosefu wa lishe bora,” alisema Mlali.
 
Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Shida Masumbi alisema kuna njia tatu za uzazi wa mpango ambazo ni njia ya muda mfupi, muda mrefu na njia ya kudumu.
 
Alisema njia za muda mrefu ni kitanzi, kipandikizi na njiti, njia za muda mfupi ni sindano, vidonge na kondomu.
 
“Pia ipo njia ya kudumu ya uzazi wa mpango ambayo ni mume na mke kufunga kizazi.
 
“Baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango husababisha maudhi kwa kukosa hedhi, kuongezeka siku za hedhi au kuona matone madogomadogo ya damu,”alisema Masumbi.
 
Alisema pamoja na maudhi hayo lakini kuna faida ambazo ni kuzuia vifo kwa mama na mtoto, mama kupumnzika kwa muda mrefu na kujishughulisha na kazi nyingine za kimaendeleo.
 
Masumbi alisema mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa na wanaume 300 walijitokeza kufunga kizazi kwa mwaka jana.

UZINDUZI WA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU LA TANZANITE MJINI ARUSHA



























ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MAISARA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara  kwa ajili ya harakati zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili kujikinga na maradhi ya Malaria.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.

Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea kuwa tishio  kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua  760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za Zanzibar.

Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.

Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza Matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia mazizini na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
Vikundi vya mazoezi vikiwa katika matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia Maisara Mjini Unguja.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba kwenye maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la Wawakilishi ilipambana na Wizara ya Afya ambapo Afya ilipata ushindi.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.