Mfanyabiashara maarufu wa kiarabu Dk. Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya
African Lyon ambayo itashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
Mmiliki wa klabu ya African Lyon,
Rahim Kangezi alisema kuwa waliamua kumuomba Al Fahim kuwa kushika
nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika michezo hasa mpira wa
miguu mbali ya kuwa mfanyabiashara bilionea katika nchi za Uarabuni
na duniani kwa ujumla.
Kangezi alisema kuwa Al Fahim ni
Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate Development ya Dubai na
miaka ya nyuma alikuwa msemaji wa kampuni inayomiliki klabu tajiri
duniani, Manchester City, Abu Dhabi United Group (ADUG). ADUG
ilinunua Manchester City mwaka Septemba, 2008.
Pia Al Fahim alitaka kununua klabu
ya Portsmouth ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya Uingereza, lakini
mpango huo haukuweza kukamilika.
Kangezi alisema kuwa Al Fahim
ataanza kazi rasmi Aprili 16 ambapo atatangaza timu yake ambayo
atafanya nayo kazi katika kuibadili klabu hiyo na kuwa klabu bora
Tanzania na Bara la Afrika.
Alisema kuwa uwepo wa Al Fahim
kuitaifanya timu hiyo kuwa na uongozi bora wenye kujua uendeshaji wa
kisasa katika masuala ya mpira kwa kuzingatia uzoefu wa mfanya
biashara huyo mzoefu katika soka na michezo mengine.“Haikuwa kazi
rahisi Al Fahim kukubali kuingia kwenye uongozi wa klabu yetu, ila
tunashukuru kwani alituelewa baada ya kukutana naye alipokuja hapa
nchini kwa shughuli zake, “ alisema Kangezi.
Alisema kuwa lengo lake ni kuona
African Lyon inakuwa klabu ya mfano sit u kwa Tanzania, hata kwa nchi
za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Kangezi alisema kuwa
mipango yao ya awali ni kuhimarisha timu ya kwanza ili iweze kufanya
vyema katika mashindano ya ligi kuu na pia kuanzisha msingi mzuri wa
timu za watoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni