Mkurugenzi
 Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu 
(UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa 
zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa
 PSSN wa TASAF. (Picha na Modewjiblog)
Washirika
 wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito 
vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya 
masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na 
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa 
wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
Washirika
 hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
 Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa 
la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF 
katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).
Wakitoa
 taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha 
Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao 
tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.
Walisema
 kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada 
walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia 
kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.
“Kuna
 mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama 
wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF 
kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
Mratibu
 TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa 
washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na 
Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya 
kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo 
zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia
 ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez 
alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na 
wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.
“Tunaangalia
 changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama 
Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi 
licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,
“Mpango
 huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza
 kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea 
katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema 
Rodriguez.
Kiongozi
 wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika
 ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), 
Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
Wanufaikaji wa mpango wa PSSN wakisoma risala kwa wageni.
Mmoja wa wanufaikaji wa mpango wa PSSN akitoa maoni wakati wa mkutano na washirika wa maendeleo waliotembelea kijiji chao.
Mwenyekiti kijiji cha Vikuge, Vitus Mchami akitoa salamu kwa niaba ya wanakijiji kwa ugeni huo.
Baadhi ya wanakijiji cha Vikuge wanaonufaika na mradi wa PSSN waliohudhuria mkutano huo.
Zoe
 Glorious (kulia) kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa 
nchini akifanya mahojiano na Mnufaikaji wa kijiji cha Vikuge, Bi. Halima
 ambaye aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kuanzisha biashara ya kufuga 
bata ambayo imemuwezesha kuendesha maisha yake na kumuingizia kipato.
Bi
 Halima akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wake wakati wa ziara ya 
washirika wa maendeleo nchini walipomtembelea nyumbani kwake.
Mwakilishi
 wa Ubalozi wa Finland nchini, Milma Kettunen (kulia) akinunua moja ya 
bidhaa iliyotengenezwa na ukili kutoka kwa wakinamama wa kijiji cha 
Vikuge walionufaika na mpango wa PSSN na kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi
 Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu 
(UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa 
zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa
 PSSN wa TASAF.
Mwakilishi
 wa USAID, Daniel Moore akinunua kitamba cha Batiki kutoka kwa 
wanufaikaji wa mpango wa PSSN unaoendeshwa na TASAF wakati wa ziara ya 
kukagua miradi mbalimbali ya TASAF mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
 Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa 
Dabo  (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Eric 
Beaume wakimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Vikuge aliwezeshwa na 
mpango wa PSSN na kufanya biashara ya kilimo cha matunda na mazao 
mbalimbali. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Vikuge,Vitus Mchami, 
anayefatia Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare
Baadhi ya Biashara za wananchi wa Vikuge walionufaika na mpanngo wa PSSN wa TASAF.
Baadhi ya wanakijiji wa Mwanabwito, Kibaha mkoa wa Pwani waliohudhuria mkutano wa washirika wa maendeleo.
Mratibu
 TASAF wa wilaya ya Kibaha, Goodson Hare akizungumza jambo wakati wa 
kutizama biashara zinazofanywa na wajasiriamali walionufaika na mpango 
wa PSSN wa TASAF kutoka kijiji cha Vikuge, Kibaha.
Ujumbe
 wa washirika wa maendeleo nchini akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
 Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo  (kulia) 
wakiwasili kwenye kijiji cha Mwanabwito.
Ujumbe
 wa washirika wa maendeleo nchini na viongozi wa TASAF katika picha ya 
pamoja walipotembelea shamba la miti katika kijiji cha Mwanabwito mkoani
 Pwani.
Afisa
 Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia 
Nkhoma- Ledama (katikati) akifafanua jambo kwa baadhi ya wajumbe wa 
msafara wa washirika wa maendeleo nchini wakati wa ziara hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni