JUMLA ya washindi 12
wamepewa tiketi za bure za safari ya ndege katika shindano lililodhaminiwa na
Festjet Tanzania.
Tiketi hizo ambazo
zitawawezesha kusafiri katika ndege ya garama nafuu ndani ya ndani na nje ya
nchi ambako Fastjet husafiri, ni sehemu ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya
Fastjet wakati wa msimu wa sherehe za Pasaka ziliyomalizika wiki iliyopita.
Akizungumza wakati wa
sherehe ya kutoa zawadi hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano
na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro alisema kuwa shirika la Fastjet limechukua
hatua ya kudhamini wateja wake kwa kuwapa zawadi hizo za tiketi za bure ikiwa
ni sehemu ya majukumu yake ya kurudisha shukrani kwa wateja wake ambao wamekuwa
watiifu kwa shirika hilo.
“Katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita, kampuni ya fastjet imekuwa ikitoa huduma bora za safari
ya anga ambazo ni salama, zenye uhakika na kuaminika kwa wateja wake ambao hadi
sasa wamefikia abiria milioni 1.8”, alisema Mbogoro.
Aliongeza na kusema
kuwa, “tunaimani kubwa na wateja wetu kwa ushirikiano wao waliouonyesha pamoja
na sisi katika kipindi hicho chote na kutokana na hali hiyo, fastjet imeamua
kutoa zawadi ya tiketi za bure kwa baadhi yao ili wasafiri kwenda kokote kule
ndani na nje ya nchi”, Mbogoro aliongeza.
Alisema kuwa tiketi
hizo zitawawezesha washindi wao kusafiri na wenzi wao ili kufurahia msimu huu wa
sikukuuu ya pasaka na wapendwa wao wakiwemo marafiki na jamaa zao.
Aliongeza kuwa, washindi
hao walichaguliwa baada ya kutoa majibu sahihi wakati wa maswali yaliyofanyika
kwa njia ya mahojiano ya vyombo vya habari nchini.
“Washiriki katika
shindano hili walikuwa wengi mno, na kati yao 12 pekee ndio waliofaulu na jopo
la majaji kuwachagua kama washindi”, Mbogoro alifafanua.
Katika mahojiano, mmoja
wa washindi wa zawadi hii, Ally Sangawe, alisema: “ Naishukuru fastjet kwa
kuandaa shindalo hili kwa kuwa sasa nitaweza kusafiri kwa kutumia tiketi hii ya
bure na kufurahia wikiendi njema na mpenzi wangu. Hii ni fursa ya kipekee na
ambayo ni muhimu kwangu”.
Karim Lungu, ambaye pia
ni miongoni mwa washindi, alitoa rai ya furaha kwa waandaaji wa shindano hilo
na kusema kuwa, “sasa kwa kuwa nilikuwa na hamu ya kusafiri kwenda Mwanza ambapo
hapo awali sikuwa na uwezo wa kukata tiketi, na sasa
nashukuru
kupata tiketi ya bure ambayo sasa imeniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kufika
huko”.
Mbali na kusafiri ndani
ya nchi kila siku katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro,
Mbeya na Zanzibar, Mbogioro alisema kuwa Fastjet husafiri na kutua katika mji wa
Johannesburg-Afrika ya Kusini, na pia kampuni ilizindua safari ya moja kwa moja
kwenda Nairobi-Kenya na sasa imeongeza maradufu safari za kila siku, kutoka
mara moja kwa wiki na kwenda mara mbili kwa wiki ndani ya miji hii miwili iliyo
mikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni