Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati Ardhi na Makaazi Ali Khalil Mirza na
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Multiconsult ya Norway Oyvi’nd Holtedahl
wakipongezana mara baada ya kusaini Mradi wa kuimarisha huduma za umeme
Zanzibar.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji , Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza,
akitoa maelezo juu ya mradi wa kuimarisha huduma za Umeme Zanzibar,
kabla ya kutiliana saini makubaliano ya miaka mitatu na nusu na Serikali
ya Norway katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara Forodhani
Mjini Zanzibar.
Mshauri
mwandamizi wa Kampuni ya Multiconsult ya Norway Andrew Yager akitoa
shukurani kwa Serikali ya Zanzibar kwa kuichagua kampuni yao katika kazi
za kuimarisha huduma ya umeme katika hafla ya kutilina saini
makubaliano ya mradi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati Ardhi na Makaazi Ali Khalil Mirza
(wa kwanza kulia waliokaa) na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Multiconsult
ya Norway Oyvi’nd Holtedahl wakitia saini makubaliano ya kuimarisha
huduma za umeme Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya
Wizara, Forodhani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga, Maelezo Zanzibar.
Na Miza Othman-Melezo Zanzibar
SERIKALI
ya Mapinduzi Zanzibar, imetiliana saini na Serikali ya Sweden
makubaliano ya kuimarisha huduma za nishati ya umeme hapa nchini.
Katika
hafla ya utiaji saini wa mradi huo, Zanzibar iliwakikishwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza,
wakati Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Multi Consult kutoka
Norway Oyvind Holtedahl, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Sweden.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati
na Makaazi Katibu Mkuu Mirza, alisema kampuni ya Multi Cionsult
ilishinda zabuni hiyo kati ya kampuni 12 zilizoomba kutekeleza mradi
huo.
Alieleza kuwa mradi huo utakaochukua miaka mitatu na nusu
hadi kukamilika kwake, utagharimu shilingi bilioni 12.7 za Kitanzania.
Amefahamisha
kuwa, miongoni mwa matumizi ya fedha hizo, ni kuwapatia mafunzo
wafanyakazi wa wizara hiyo ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti ili
wafanye kazi zao kwa ufanisi.
Mirza alieleza kuwa, lengo la
Kampuni hiyo ni kusaidia katika kulijengea uwezo Shirika la Umeme
Zanzibar (ZECO) pamoja na Idara zake kuhusu sera ya nishati ambayo ni
muhimu kwa maenedeleo ya taifa.
Naye Mshauri Mwandamizi wa
Kampuni ya Multi Consult ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na ameahidi kuwa wataitekeleza kwa
ufanisi mkubwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni