Baadhi
ya Nyumba za makazi, huduma mbalimbali na vijiwe vya kufanyia biashara
eneo la Chalinze nyama Dodoma vikiwa vimezingirwa na maji (mafuriko)
kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo usiku wa kuamkia April 4,
2016.
Baadhi
ya Wakazi wa eneo la Chalinze nyama Dodoma wakihamisha mali zao baada
ya makazi yao kuzingirwa na maji (mafuriko) kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha mkoani humo usiku wa kuamkia April 4, 2016.
Baadhi
ya magari ya kubeba abiria mapema yalinusurika kusombwa na
mafuriko yalipojaribu kuvuka barabara eneo la Chalinze nyama Dodoma
kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa
kuamkia April 4, 2016.
Safari
za magari ya abiria na mizigo zilikwama eneo la Chalinze nyama Dodoma
kwenye barabara itokayo Dodoma kuelekea Dar es salaam kuanzia alfajiri
ya Aprili 4, 2016 hadi alasiri kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na
mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Chamwino Mhe. Farida Mgomi (katikati) na viongozi wengine wakikagua eneo
la Barabara eneo la Chalinze nyama ili kuona namna ya kupitisha magari
ya abiria na mizigo yaliyokwama tangu alfajiri ya Aprili 4, 2016 hadi
alasiri kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha
usiku wa kuamkia siku hiyo.
Magari
ya abiria na mizigo yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 1,000 ambayo yalikwama
eneo la Chalinze nyama Dodoma kwenye barabara itokayo Dodoma kuelekea
Dar es salaam kuanzia leo alfajiri hadi alasiri kufuatia barabara hiyo
kufungwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa
kuamkia April 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akishuhudia magari ya mizigo na
abiria yakiendelea na safari Alasiri baada ya kuruhusiwa kufuatia
kupungua kwa maji (mafuriko) yaliyofunga barabara kuu ya Dodoma Dar es
salaam eneo la Chalinze nyama Dodoma tangu alfajiri.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kushoto) akiijulia hali kaya
iliyonusurika kusombwa na mafuriko kufuatia makazi yao kuzungukwa na
maji mengi eneo la chalinze nyama yaliyosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha usiku wa kuamkia April 4, 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni